Na Doreen Aloyce,TimesMajira Online,Dodoma
TAASISI ya Tiba Asili ya Corrnwell Tanzania imempongeza Rais Dkt.John Magufuli kwa kupendekeza kuruhusiwa kwa maduka ya dawa za asili na matibabu yake.
Rais Dkt.Magufuli katika hotuba yake aliyoitoa Novemba 14, mwaka huu alipofungua Bunge la 12 jijini hapa, alisema kuwa Serikali imeruhusu maduka ya tiba asili pamoja na huduma hiyo.
Akizungumza katika kongamano la wadau wa afya nchini la Tanzania Health Summit, Mratibu wa taasisi hiyo, Elizabeth Lema amesema, Rais Magufuli amewaheshimisha kupitia hotuba yake.
“Kwa kweli namshukuru Rais Dkt.Magufuli kwa kutuheshimisha sisi watu wa tiba asili,hotuba yake aliyoitoa siku ya kuzindua Bunge la 12, ametufanya sasa tutambulike rasmi katika jamii,”amesema Lema.
Lema amesema,heshima waliyopewa na Rais Magufuli katika hotuba yake ndio iliyowapa tiketi ya kukubalika kushiriki katika kongamano la watu wa afya linalofanyiika jijini Dodoma.
Aidha, Lema amesema kuwa Tanzania ina uhitajili wa tiba asili nyingi katika misitu ya hapa nchini,hivyo Watanzania wanatakiwa wathamini vya kwao.
Mratibu huyo wa Cornwell amesema kuwa, wanaratajia kutangaza dawa za tiba asili katika maeneo mbalimbali kwani wenzao wa Asia wameenda mbali sana katika sekta hiyo.
“Nawasihi Watanzania wapendelee kutumia tiba asili kwani ni dawa ambazo hazina kemikali, ni dawa zinazotokana na mizizi,hivyo Watanzania wasiogope,”‘ameema Lema.
Aidha,Lema aliwaondoa wasiwasi wananchi wanaofananisha tiba hizo na masuala ya kichawi na kusema kuwa tiba asili si uganga wa kienyeji.
Taasisi hiyo ambayo ina matawi katika mikoa mbalimbali hapa nchini imejikita zaidi katika utengenezaji dawa hizo pamoja na kutoa huduma kwa wagonjwa.
More Stories
Bumbuli kutekeleza miradi kwa kuangalia vipaumbele
Makalla:Kupanga fujo ni dalili za kushindwa uchaguzi
Tanzania yapanda viwango Utawala wa Sheria Duniani