Na Martha Fatael,TimesMajira, Same
JESHI la Polisi mkoani Kilimanjaro limetaja majina ya watu waliofariki katika ajali eneo la Kirinjiko wilayani Same, huku idadi ya waliofariki ikiongezeka na kufikia 11.
Hata hivyo polisi imeomba wananchi kwenda kutambua miili ya watu watatu ambao hawajatambuliwa pamoja na majeruhi sita ambao hawajafahamika hadi sasa.
Kamanda wa polisi mkoani hapa, ACP Amon Kakwale amesema ajali hiyo ilitokea Aprili 13 majira ya saa 7 mchana eneo la Kirinjiko wilayani Same, ikihusisha gari aina ya Toyota Alphard na Toyota Hiace.
Amesema, Toyota Alphard yenye namba za usajili T 898 DKX ikiendeshwa na Emanuel Robert ikitokea Arusha kugongana uso kwa uso na gari namba T 806 BNM aina ya Toyota Hiace ikitokea Hedaru kwenda Same.
Waliofariki ni Joshua Philemon (60) aliyekuwa dereva wa Hiace, Juma Msuya, Adamu Msuya (52) wote wakazi wa Ugweno Mwanga, Mwajuma Haji (70) mkazi wa Hedaru.
Wengine ni Nietiwe Hemed (47), Samwel Julius (44) mkazi wa Gonja Maore Same na Amon John (52) mkazi wa Same.
Miili mingine ni Ngai Walter (50) mkazi wa Same na wengine wawili ambao hawajatambuliwa ambapo mmoja mwenye umri wa kati ya miaka 35 hadi 38.
Majeruhi ni Amina Salehe(55) mkazi wa Kirinjiko, Emanuel Robart (34) mkazi wa USA River Arusha, Nelson Aminiel (45) mkazi wa Arusha, Frank Japhet (20) mkazi wa Moshi, Anthony Mkomba(27) Utingo wa Hiace mkazi wa Mgagao wilaya ya Same.
Majeruhi wengine ni Mariam Iddy mkazi wa Kirinjiko huku wengine sita wakiwa hawajafahamika na wanaendelea na matibabu katika hospitali za wilaya ya Same pamoja na KCMC.
Kakwale alisema, chanzo cha ajali ni kupasuka kwa gurudumu la nyuma upande wa kulia wa Toyota Alphard kupasuka na kuhamia upande wa kulia na kugongana na Toyota Hiace na kusababisha vifo na majeruhi hao.
Kakwale alitaka madereva kuendesha magari kwa tahadhari ili kuweza kukabili dharura zozote ambazo zitajitokeza barabarani.
More Stories
ITA chatakiwa kutoa mafunzo ya viwango vya juu na kasi ya maendeleo ya Kisayansi
Wagombea CHADEMA wakipewa ridhaa,watakuwa wawazi
TTCL yafanya maboresho katika huduma zake