Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
JUMLA ya Walimu 172 Mkoa wa Dar es Salaam wamepata ajira mpya ya Ualimu mwaka huu wa fedha wa FEDHA 2022/23.
Hayo yalisemwa na Afisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam Abdul Maulid wakati wa kuzungumza na waandishi wa Habari.
Mwalimu Maulid alisema mwaka huu wamepokea Walimu wapya 172 wanatarajia kuanza kazi rasmi waweze kulipoti katika vituo vyao vya kazi
“Serikali imewapa ajira Walimu wapya 172 ambao wataanza kazi hivi Karibuni Katika Walimu wapya 172 Walimu wa shule za msingi 37 na Walimu wapya wa shule za Sekondari 135 wataongeza nguvu Katika Walimu wa zamani”alisema Mwalimu Maulid.
Alisema Walimu wa awali wa mkoa Dar es Salaam jumla Walimu wa Shule za Msingi 11660 na Walimu wa Shule za Sekondari 5645.
Alisema Serikali imetimiza wajibu katika sekta ya elimu imewekeza vizuri katika ujenzi wa madarasa ya shule za msingi na shule za Sekondari Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametekeleza kwa vitendo sera ya Elimu bira malipo.
Aliwataka Walimu wa Shule za Msingi na Sekondari Katika mkoa Dar es Salaam wasichangishe fedha kwa Wazazi,shule itakayochangisha michango
Walimu wakuu watachukuliwa hatua.
Katika hatua nyingine Afisa Elimu mkoa Dar es Salaam aliwataka Wazazi Mkoni Dar es es Salaam kufatilia Maendeleo ya watoto wao shuleni kila wakati Kwa kushirikiana na walimu .
More Stories
Ujenzi wa Hospitali ya rangitatu wafikia asilimia 69
Wafanyabiashara wakutana Dar,kujadili hali ya biashara
Kongamano la Uwekezaji kati ya Tanzania na Ubelgiji lafanyika Dar