Na Hadija Bagasha Tanga, TimesMajira Online
Kamishina Jenerali wa mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya nchini Gerald Kusaya amewaagiza walimu wa shule za msingi kutoka mikoa 12 ya Tanzania bara na visiwani Zanzibar waliopatiwa mafunzo na chama cha Scouts kwenda kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya kupitia elimu watakaokuwa wakitoa katika makundi mbalimbali ikiwemo ya wanafunzi.
Kusaya ametoa maagizo hayo alipofika Mkoani Tanga wakati akitoa semina kwa walimu wa shule za msingi ambapo alisema kuwa bado tatizo la matumizi ya dawa za kulevya ikiwemo bangi ni kubwa hivyo kuwataka kwenda kutumia nafasi zao katika kuelimisha makundi mbalimbali sambamba na kushirikiana kutoa taarifa kwa mamalaka husika vikiwemo vyombo vya ulinzi na usalama.
Hata hivyo alitaja uwepo wa bandari bubu hapa nchini , ukanda wa bahari ambapo amesema licha ya kuwepo kwa vyombo vya ulinzi na usalama katika maeneo hayo bado hivyo pasipo jitihada za makusudi kuchukuliwa na ushirikiano kutoka kwa jamii tatizo la madawa ya kulevya hapa nchini halitoweza kupungua au kuondoka kabisa.
“Dawa za kulevya zinaathiri vitu vingi kwahiyo niwaombe sana tusaidiane kutoa taarifa na mapambano ya kuzuia na kupiga matumizi ya madawa ya kulevya kuna changamoto ya uelewa mdogo katika jamii juu ya madhara ya madawa ya kulevya ikiwemo bangi kwahiyo la msingi tuendelee kuelimishana kutoa taarifa kwa mamalaka husika” alisema Kusaya
Aidha kusaya alisema bado jitihada mbalimbali zinaendelea kuchukuliwa na serikali ili kudhibiti uingiaji na matumizi ya madawa ya kulevya hapa nchini ambapo kwa mwaka 2021/2022 mamlaka hiyo imefnikiwa kukamata tani 23.48 za bangi na tani 14.5 za Mirungi kuwa nyakati tofauti.
“Scouts ni jeshi kubwa na kila unapogusa sehemu ya nchi hii utakutana na Scout hasa vijana ambao ndio waathirika zaidi wa madawa ya kulevya, tatizo la madawa ya kulevya ni kubwa sana zinazotokea nje ya nchi kuja hapa kwetu na hata sisi wenyewe tunasafirisha tunajua madhara makubwa yanayotokana na madawa ya kulevya ukitanzama kwa ujumla wake tanzania tuna wahanga zaidi ya laki tano na kila mmoja ni muathirika hata kama hutumii lakini utaguswa kwa namna yeyote ile” alisema Kusaya.
Awali akifungua semina ya siku tano inayotolewa na chama cha scout Tanzania kwa walimu wa shule za msingi naibu waziri wa wizara ya elimu Sayansi na teknolojia Omari Kipanga amewaagiza walimu waliopatiwa mafunzo ya Scouts kwenda kuanzisha vikundi vingi zaidi vya chama hicho kwa lengo la kuendelea kudumisha uzalendo uwajibikaji pamoja na kuendelea kupiga vita matumizi ya madawa ya kulevya ambayo yamekuwa yakipoteza nguvu kazi ya Taifa.
Aidha Waziri Kipanga aliwataka walimu hao pamoja na chama cha Scouts Tanzania kwenda kuyatumia mafunzo hayo kufundishia nyimbo za kizalendo ikiwemo wimbo wa Taifa na wa Afrika mashariki kwa lengo la kuendelea kurithisha na kuendeleza utaifa kwa vizazi vijavyo.
“Kuteuliwa kuja kupata mafunzo haya mkiwakilisha halmashauri zenu nendeni mkafundiahe katika kukuza uzalendo na tutafwatilia kwa karibu kufanya tathmini kuona mna enda kuyafanyia kazi nawaagiza kila Mwalimu aliyepata mafunzo haya akaanzishe vikundi vya Scouti mashuleni ili kuwafanya vijana wetu kuwa wazalendo kuheshimu nyimbo zatu ikiwa wimbo wa Taifa na Afrika mashariki”
“Vijana wetu wamekuwa wahanga wakubwa wa madawa ya kulevya naomba mjue kuwa vijana wetu wanaharibika na badala yake kuwapongeza kabisa tumieni mafunzo hayo kueleza athari zake kwahiyo tuna Kazi kubwa ya kufanya ” alisema Kipanga
Akizungumza Mkuu wa chama cha scout Tanzania Mwantumu Mahiza alisema kuwa kwa kushirikiana na wizara ya elimu tumeamua kutoa mafunzo kwa walimu wa shule za msingi na sekondari lengo ni kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2023 kikao shule iwe na Mwalimu wa scauts ili kuendelea jules vijana katika maadili uzalendo na uwajibikaji.
“Tunazo shule za msingi na sekondari taktibani 2350 na sisi scaut tulikabidhiwa jukumu la kuwalea vijana katika maadili yaliyo mema hatuwezi kusema kwamba wakufunzi wa scauts pekee wataweza kuzifikia shule hizi.
“Tunazo shule za msingi na sekondari taktibani 2350 na sisi scaut tulikabidhiwa jukumu la kuwalea vijana katika maadili yaliyo mema hatuwezi kusema kwamba wakufunzi wa scauts pekee wataweza kuzifikia shule hizi hivyo tuliamua kwa pamoja kutoa mafunzo kwa walimu na sasa tuko awamu ya pili lengo ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2023 kila shule ya msingi na sekondari iwe na Mwalimu mlezi kwa kufanya hivyo tumeona tuongeze Kasi zaidi” alisema Mahiza.
Alisema kuwa kufanya hivyo wataendelea kuwalea na kuwakuza vijana na jamii kwa ujumla katika uzalendo uadilifu upendo na mshikamano na wenye kukupenda kuulinda na kuitumikia nchi ya Tanzania huku akiwataka walimu wote waliopatiwa mafunzo hayo kwenda kuyafanyia Kazi kwa kuwajibika zaidi.
“Walimu hasa watakapomaliza mafunzo watakuwa wamepata maadili na wasifu wa scout uzalendo uadilifu na utiifu na uaminifu ikiwemo kupambana na madawa ya kulevya kwahiyo wanatakiwa wakawe wazalendo na wenye kukupenda sitarajii walimu waliokuwa kiapo cha Scout wakakengeuke ” aliongeza
Kwa upande wao baadhi ya walimu walioshiriki semina hiyo akiwemo Rehema Masayanyika na Rajabu Sakasa waliahidi kwenda kuyatumia mafunzo hayo ya Scouts waliyoyapata kubadilisha maadili na matazamo wa jamii wakiwemo vijana kuhakikisha wanaumarisha uzalendo uwajibikaji na uadilifu sambamba na kupambana na madawa ya kulevya.
More Stories
Madiwani Korogwe TC wahakikishiwa maji ya uhakika
CHADEMA wampongeza Mkurugenzi Mpanda
Ukosefu wa maji wasababisha wanafunzi kujisaidia vichakani