Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Kufuatia katazo wa Waziri wa TAMISEMI Innocent Bashungwa kuhusu sakata la bodaboda na bajaji kuingia mjini, Walemavu na Bodaboda wameandamana mpaka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam wakishinikiza Waziri Kutengua tamko alilotoa.
Hatua ya Walemavu na Bodaboda kuandamana imekuja Kufuatia Tamko la Waziri Bashungwa kukinzana na Makubaliano ya pamoja na utaratibu mzuri uliokuwa umewekwa tangu mwanzo baina ya Waendesha Bajaji Wenye ulemavu na Waendesha bodaboda.
Miongoni mwa Makubaliano hayo ni pamoja na Bajaji za watu Wenye ulemavu kuruhusuwa kuingia katikati ya mji na kuegesha kwenye Vituo vitatu walivyopangiwa, Bajaji za wasio na ulemavu kutoruhusiwa kuingia katikati ya mji, Bodaboda zilizosajiliwa na kukidhi vigezo kuruhusuwa kuegesha kwenye Vituo Saba katikati ya mji na Bodaboda zisizokuwa na Vibali kuruhusiwa kuingia mjini Kwa kigezo Cha kushusha abiria na kugeuza.
Katika jitiada za kutuliza maandamano hayo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amelazimika kufanya mawasiliano ya simu na Waziri Bashungwa na kumuelezea Hali halisi ya maandamano hayo na madai ya waandamanaji kushinikiza kutumika kwa utaratibu waliokuwa wamejiwekea awali ambapo Baada ya kuridhika na utaratibu mzuri uliokuwa umewekwa, Waziri Bashungwa ameridhia kuendelea kwa utaratibu uliokuwa ukitumika awali wa Pikipiki na Bajaji kuingia Katikati ya mji Kwa mujibu wa makubaliano na maridhiano ya pamoja yaliyokuwa yamewekwa baina ya Waendesha Bajaji Wenye ulemavu na waendesha bodaboda.
Uamuzi huo umepokelewa kwa mikono miwili na Wandamanaji hao ambao wameahidi kuendesha Shughuli zao pasipokuvunja makubaliano na utaratibu wa pamoja waliokuwa wamejiwekea awali kwakuwa umehusisha na kukidhi matakwa ya pande zote.
More Stories
Mjumbe wa Baraza UWT ahimiza wananchi kuwachagua viongozi wa CCM
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â