Na Moses Ng’wat,Timesmajiraonline,Songwe.
MKUU wa Mkoa wa Songwe, Dkt. Francis Michael, amewataka wakuu wa Wilaya na wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri kwenda kusimamia ipasavyo zoezi la Chanjo ya Polio ili kuleta matokeo chanya kwa kuhakikisha Watoto wote 402,644 walio chini ya miaka nane ndani ya Mkoa huo wanapatiwa Chanjo hiyo .
Ametoa maelekezo hayo leo Septemba 14, 2023 katika kikao cha wajumbe wa kamati ya huduma ya Afya ya Msingi waliokutana kwa lego la kupanga mikakati ya namna ya uendeshaji wa zoezi hilo la Chanjo linalotarajia kuanza septemba 21 hadi 24 Mwaka huu wa 2023.
Mkuu huyo wa Mkoa Dkt. Francis amesema kuwa sanjari na Mkoa wa Songwe, kampeni hiyo maalum ya utoaji chanjo dhidi ya ugonjwa wa polio ambayo itatolewa kwa watoto wote wenye umri chini ya miaka nane itahusisha pia mikoa mingine ya Mbeya, Rukwa, Katavi, Kigoma na Kagera.
“Tunamshukuru Mganga Mkuu wa Mkoa kwa kikao hiki kwani Waziri wa Afya (Ummy Mwalimu) aliagiza tufanye kikao hiki, hivyo ninachotaka kila kiongozi hasa Ma-dc na Ma-ded wajue na kwenda kusimamia ipasavyo zoezi hilo,”amesema Dkt. Francis.
Awali akiwasilisha taarifa ya kampeni ya Chanjo ya polio kwenye kikao hicho cha kamati ya Afya ya Msingi, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Dkt. Boniface Kasululu amesema lengo la kikao hicho ilikuwa ni kujenga uelewa kwa wanajamii kuhusu faida za Chanjo ya polio .
Dkt. Kasululu amesema kampeni hiyo itaendeshwa na Wizara ya Afya ikishirikiana na shirika la Afya Dunian (WHO), shirika la kuhudumia Watoto (UNICEF) pamoja na wadau wengine.
Akizungumzia kuhusu namna ya zoezi hilo litakavyofanyika , Mganga Mkuu Dkt. Kasululu amesema kampeni hiiyo ya Chanjo itafanyika kupitia vituo vyote Vya kutolea huduma za Afya nawatoa huduma watapita Nyumba kwa Nyumba na mahali popote ambapo Mtoto anaweza kuwepo.
Dkt. Kasululu amesema sanjari na kampeni hiyo ya Chanjo ya polio, zoezi hilo pia litahusisha kuwatafuta Watoto wote waliochini ya miaka 15 ambao wamepata ulemavu wa grafia (washukiwa wa polio) na kutoa taarifa vituo vya karibu kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
More Stories
Prof. Mwakalila asisitiza uadilifu, uzalendo kwa wanafunzi wapya chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere
Benki ya Equity Tanzania yasaini mkataba wa kuwawezesha wanawake kiuchumi
Rais Samia alivyoguswa kifo cha msanii Grace Mapunda