Na Joyce Kasiki,Dodoma
MWENYEKITI wa uwezeshaji wa Ndani na Ununuzi wa pamoja pia ni Mwenyekiti wa Mbolea ya ruzuku kitaifa Louis Kasera amewaasa wakulima kujisajili mapema ili wapate mbole ya ruzuku itakayowawezesha kuzalisha mazao kwa tija.
Akizungumza na waandishi wa habari kwwnye maonesho ya wakulima na wafugaji (88) kwenye banda la Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea nchini (TFRA) amesema malengo ya setikali ni kuandikisha wakulima milioni saba lakini mpaka sasa waliojisajili ni wakulima milioni nne tu.
Hata hivyo amesema hadi ifikapo mwishoni mwa mwaka msimu wa kilimo ujao wawe wamefikia idadi iliyotarajiwa.
Aidha amesema kwa ambao walishajisajili kipindi cha nyuma wanapaswa kuuhisha taarifa zao kwa alama za vidole ili mkulima ajulikane alipo lakini pia ijue mkulima huyo ni nani.
“Ninachoomba wakati wa kujisajili na kuuhisha taarifa zao,watoe taarifa sahihi ili waweze kufikiwa walipo.”amesema Kasera
Vile vile amesema mbolea ipo ya kutosha hivyo amewaasa wakulima wanunue mbolea mapema ili kuangalia kwenye mapungufu ipelekwe huko.
“Kwa sasa msimu ndiyo umeanza lakini tuna tani 300,000 za mbolea ya kupandia na kukuzia .”amesema Kasera
Kwa mujibu wa Kasera,hali ya mbolea ni ya kutosheleza huku akisema mwaka huu lengo ni kufikia tani milioni moja na kwamba asilimia 30 tayari ipo ndani ya nchi na bado kuna meli zipo njiani zimebeba mbolea .
“Hadi Disemba zote zitakuwa zimesgaingia,na hizo ni zile zinazotoka nje ,bado zinazozalishwa katika viwanda vyetu vya ndani.”amesema
Kasera amesema ,hapa nchini kuna viwanda viwili cha Minjingu na Itracom ambavyo vina uwezo wa kuzalisha zaidi ya tani 850,000.
“Matarajio ya kiwanda cha Itracom ni kuzalisha tani zaidi ya laki sita,na Minjingu tani zaisi ya 250,000 ,kqa hiyo utaona viwanda vya ndani uzalishaji wake ni zaidi ya asilimia 50 ,lengo la serikali ni kuondoa utegemezi ,tunataka ifikapo 2030 tuwe tunajitosheleza kwa mbolea ya ndani.”amesisitiza
More Stories
Zaidi ya wananchi 32,000 Vijiji vya Wilaya za Morogoro na Mvomero kuanza kupata mawasiliano
Wafanyabiashara waomba elimu ya namna watakavyorejea soko kuu
DCEA,Vyombo vya Ulinzi na Usalama vyafanya operesheni ya kihistoria