November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wakulima wa Mpunga Madibira wampa tano Rais Samia mradi wa REGROW

Na Mwandishi wetu, timesmajira

WAKULIMA wa Mpunga Kata ya Madibira wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya wameishukuru Serikali ya Rais wa Awamu ya Sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa utekelezaji wa Mradi wa Uboreshaji wa mifereji ya Umwagiliaji Mashamba ya Mpunga Madibira kupitia Mradi wa Kuboresha Usimamizi wa Maliasili na Kukuza Utalii Kusini mwa Tanzania REGROW, kwa kuwa mradi huo unawawezesha kulimima mpunga kwa huwakika wa kupata mavuno wanayotarajia.

Wakulima hao wametoa pongezi hizo kwa Rais Samia akiwa anatimiza miaka mitatu tangu aanze kuiongoza Serikali ya Awamu ya Sita ambapo wameeleza kuwa mradi huo umeanza kuwaletea tija kwani kwasasa wakilima Ekari mbili na nusu wanapata tani 12 hadi 15 ambapo zamani walikuwa wakipata tani nne mpaka mpaka tani saba kutokana na changamoto ya ukosefu wa maji ya uhakika.

Aidha wanufaika wa mradi wa umwagiliaji wa Skimu ya Umwagiliaji ya Madibira inayotekelezwa kupitia REGROW chini ya Wizara ya Maliasili ambapo wananchi wanaishukuru serikali kwa kutimiza ahadi ya uendelezaji kilimo cha umwagiliaji chenye matumizi rafiki ya maji.

Kadhia ya ugomvi wa mara kwa mara huku wakiwa wamebeba silaha aina ya panga kuyatafuta maji wameondokana nayo na na kukiri kuwa utekelezaji wa mradi huu umesaidia upatikanaji maji ya uhakika na kuweza kuendesha kilimo wakiyasubiria kwa shahuku kubwa mavuno yao huku amani ikitawala.

Mradi huo unatekelezwa na Wakandarasi Wazawa kutoka katika Kampuni ya Skyline Properties Limited kwa kushirikiana na White City International kuwa wataendelea kutekeleza miradi kwa kiwango kimachopaswa huku Mhandisi wa Umwagiliaji skimu ya Madibira Njanji Mlwale amesema ufanisi katika kusafirisha maji utakuwa bora kuliko kipindi cha nyuma.