September 28, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wakazi Uvinza waahidi kura za kishindo kwa Samia

Na Allan Vicent, Timesmajiraonline, Uvinza

WAKAZI wa Vijiji na Vitongoji mbalimbali katika halmashauri ya Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma wameguswa kwa kiwango kikubwa na kasi ya utendaji wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na kuahidi kumpa kura za kishindo hapo mwakani.

Wamebainisha hayo kwa nyakati tofauti walipokuwa wakiongea na mwandishi wa gazeti hili ambapo wameeleza kufurahishwa na kasi yake ya utekelezaji miradi ya maji katika Vijiji na Kata mbalimbali ndani ya Wilaya hiyo.

Uhuru Lubambo (52) mjasiriamali mkazi wa Kitongoji cha Kamgumile Mjini Uvinza amempongeza Rais Samia kwa kuwapelekea mradi wa maji uliogharimu mamilioni ya fedha na kumaliza kero iliyodumu kwa miaka mingi.

Amesema kuwa mradi huo licha ya kuwawezesha kupata huduma ya maji safi na salama ya bomba kwa ajili ya kunywa na matumizi ya nyumbani pia maji hayo yamemsaidia kustawisha bustani ya miti ya matunda ambayo humpa kipato.

Amefafanua kuwa bustani hiyo imemwezesha kupata zaidi ya sh laki 4 kila mwezi kwa kuuza miti ya matunda na kivuli anayootesha na kumwagilia kwa kutumia maji yaliyoletwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA).

‘Tunamshukuru sana Rais Samia kwa kutuletea Viongozi wachapa kazi ambao wanasimamia ipasavyo miradi ya maji, kuanzia Waziri mwenye dhamana ya Maji Jumaa Awesu, Mkuu wa Wilaya na Meneja wa RUWASA wa Wilaya’, amesema.

Bi Stella Kanonko (42) mkulima, mkazi wa Kijiji cha Kazuramimba ameeleza kuwa miradi ya maji iliyoletwa na Rais Samia imewapunguzia adha ya kunywa maji machafu na kutembea umbali mrefu kwenda kuchota maji ya mtoni.

‘Tunajivunia kuwa na Rais mwanamke, anayejali maisha ya wananchi, tulikuwa tunateseka sana kubeba ndoo za maji kichwani kutoka mtoni au mabondeni, akinamama wa Uvinza tumeshaamua, mwakani tunampa kura zote’, amesema.

Mwanachama wa Umoja wa Wanawake (UWT) wa CCM Wilayani humo Yasinta Ntabirwa amepongeza kazi nzuri inayofanywa na Rais Samia ya kutekeleza miradi ya maji mijini na vijijini kwani imesaidia sana kutatua kero ya maji kwa wananchi.

Amebainisha kuwa wakazi wengi wa Mji wa Uvinza walikuwa wanategemea sana maji ya Mto Luchugi na Malagarasi kwa kunywa lakini sasa kupitia RUWASA wananchi wengi wanapata maji nyumbani kwako au karibu na maeneo yao.

Amewataka akina mama na wakazi wote wa Wilaya hiyo na Mkoa mzima kumuunga mkono Rais Samia atakapochukua fomu ya kugombea urais hapo mwakani ili amalizie miaka yake mitano kwa mafanikio makubwa.

Mwishopppppppppppppppppppppp