Na Allan Vicent, TimesMajira Online
WAKALA wa Majisafi na Usafi wa Mazingira (RUWASA) Wilayani Kibondo Mkoani Kigoma wamefanikiwa kufikisha huduma ya maji safi na salama kwa wakazi 245,000 kati ya wakazi 315,000 wa Wilaya hiyo.
Hayo yamebainishwa jana na Meneja wa Wakala huo Wilayani hapa Mhandisi Mohamed Almas alipokuwa akiongea na Waandishi wa Habari ofisini kwake.
Amesema mafanikio hayo yametokana na kukamilika kwa miradi ya maji katika vijiji 35 kati ya vijiji 50 vilivyosajiliwa wilayani humo.
Ameongeza kuwa hadi sasa jumla ya miradi 6 inaendekea kutekelezwa na mingine 3 itaanza kutekelezwa katika mwaka huu wa fedha na kukamilika kwa miradi hiyo kutawezesha wakazi wa vijiji vyote 50 kupata huduma hiyo kwa asilimia 100.
Mhandisi Almas amefafanua kuwa kukamilishwa kwa miradi hiyo kutawezesha upatikanaji huduma ya maji katika wilaya hiyo kufikia asilimia 85 hivyo ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutekelezwa kwa asilimia 100.
‘Tunamshukuru sana Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia fedha za kutosha kufanikisha utekelezaji miradi ya wananchi, kazi iendelee, ‘ amesema.
Naye Katibu wa Bodi ya Maji wilayani humo Constantine Shija amesema kutokana na kukamilika kwa miradi hiyo wananchi sasa wanapata huduma ya maji kwa masaa 24 katika baadhi ya vijiji.
Ameongeza kuwa baadhi ya maeneo wanatumia kadi ya lipa kabla ya kutumia (pre paid) na ile ya kawaida ya kulipia kila unapochota na wanapata huduma wakati wote.
More Stories
Jokate awapa tano vijana UVCCM maandalizi Mkutano Mkuu wa CCM
Watakaokwamisha mapato Kaliua kukiona cha moto
Dkt.Gwajima aagiza kuundwa kamati za ulinzi wa watoto