November 16, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wakazi 40,000 kufaidi maji ya Ziwa Tanganyika

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online. Nkasi

ZAIDI ya wakazi 40,000 katika vijiji saba vilivypo Nkasi, wanatarajia kufaidi maji ya Ziwa Tanganyika Bombani.

Wakazi hao wana kila sababu ya kufurahi, baada ya mradi wa maji wa Kirando utakaohudumia zaidi ya wananchi 40,000 kufika katika hatua za mwisho.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Sumbawanga (SUWASA), Mhandisi Gibon Nzowa amesema kazi zilizobaki zitakamilika ndani ya muda mfupi na majaribio ya mradi huo yataanza.

Mradi wa maji wa Kirando, unaotekelezwa na wataalamu wa sekta ya maji kwa utaratibu wa force account, unasimamiwa na SUWASA.

Pamoja na kazi nyingine mradi huo, umehusisha ujenzi wa tenki lenye uwezo wa kuhifadhi lita milioni moja na chanzo cha maji ya mradi ni Ziwa Taganyika, ambapo vijiji saba vya Nkasi vitapata huduma ya majisafi, salama na yenye kutosheleza kwa asilimia 100.