Na Mwandishi wetu, Timesmajira Online DSM
Kwa mara ya kwanza nchini Tanzania, Serengeti Lite Oktobafest ilileta pamoja vipaji vya muziki na ubunifu wa hali ya juu wa Afrika Mashariki katika fukwe za Dar es Salaam, ikitoa burudani na kuonyesha utamaduni.
Tukio hili la kipekee lilijumuisha safu ya wasanii maarufu, ikiwa ni pamoja na Nyanshiski kutoka Kenya, Jose Chameleon kutoka Uganda, Ali Kiba, Bill Nas, Chino, G Nako, na wabunifu kama vile Makeke International kutoka Tanzania, wote wakishirikiana kwenye jukwaa moja kugusa mioyo ya maelfu ya Waafrika Mashariki.
Esther Raphael, Meneja wa Chapa kwa Serengeti Lite na Serengeti Premium Lager, alisema. “Serengeti Lite Oktobafest si tu maadhimisho ya muziki na utamaduni; ni jukwaa linalowawezesha vijana wa Afrika Mashariki kupata fursa za biashara,” alisema. “Zaidi ya hayo, tamasha hili linaonyesha jinsi bia inaweza kutumika kama daraja, kuwaunganisha tamaduni na watu mbalimbali wa Afrika Mashariki kwa lugha ya muziki.
“Moja ya mambo ya kipekee zaidi ya tamasha hili lilikuwa jinsdi ilizingatia usafi wa mazingira. Rispa Hatibu, Meneja wa Mawasiliano na Uendelevu, alielezea fahari yake katika juhudi za tamasha kwa kuzingatia utunzaji wa mazingira. “Serengeti Lite Oktobafest ilikuwa tamasha lenye kutunza mazingira bila taka zozote, ambapo mazingirayalipewa kipaumbele,” alielezea.
“Timu yetu ya waokota taka ilifanya kazi kwa bidii kuhakikisha mazingira safi ni kila wakati wakati wa tamasha.”Pamoja na hayo, usalama ulikuwa ni kipaumbele cha juu, huku waandaaji wa tamasha wakishirikiana na Uber, wakitoa punguzo la asilimia 40 kwa watu wanaenda kwenye tamasha kwa safari za kwenda na kurudi Coco Beach.
Hatua hii ililenga kuzuia hatari zinazohusiana na uendeshaji wa magari wakiwa wamelewa, kuhakikisha kuwa washiriki wote walikuwa na njia salama na ya kuaminika ya usafiri.Vipaji vilivyoonyeshwa katika jukwa la Serengeti lite vilikua ni vya kipekee na hakika watu waliburudika na aonyesho ya wasanii yaliyogusa mioyo ya hadhira.
More Stories
GETHSEMANE GROUP KINONDONI yaja na wimbo wa siku yetu kwaajili ya harusi
Startimes yazindua makala ya China, Africa
Mwanasheria wa Katavi aliyetimkia kwenye muziki achaguliwa tuzo za MIEMMA