Na Jackline Martin, TimesMajira Online
Imeelezwa kuwa mwitikio wa wajasiriamali umezidi kukua katika maonesho ya biashara ya kimataifa sabasaba ndani ya Banda la SIDO ambapo wajasiriamali 135 wameshiriki mwaka huu ukilinganisha na wajasiriamali 110 mwaka Jana .
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la kuhudumia viwanja vidogo-SIDO, Sylvester Mpanduji katika maonesho hayo leo Jijini Dar es Salaam ambapo amesema katika Banda la SIDO kwa mwaka huu mwananchi atakayetembelea utapata huduma mbalimbali kama vile utoaji wa mafunzo lakini pia teknolojia na mikopo
Amesema kupitia huduma wanazozitoa wapo pamoja na wajasiriamali ambao wamefaidika na huduma zao
“Mwaka huu wajasiriamali ambao wameshiriki katika maonesho ya mwaka huu ukilinganisha na mwaka Jana utakuta kwamba mwaka huu tumepata wajasiriamali wengi zaidi wapatao 135 ambapo mwaka Jana wajasiriamali walikuwa ni 110”
“Hivyo watanzania wanaendelea kupata mwitikio wa kupata huduma za SIDO na kuweza kuanzisha viwanda vyao” Amesema
Kwa upande wa Teknolojia, Mpanduji amesema wamekuja na Teknolojia mbalimbali mahususi ya Nishati safi ya kupikia hivyo katika Banda lao Wana majiko yanayotumia Nishati safi
“Utakapotembelea itakua ni fursa kwako utakaponunua na na kuona teknolojia hizo”
Kuhusu ubanguaji korosho, Mpanduji amesema wamekuwa na Teknolojia ya kubangua korosho Moja moja kwa wakati mmoja ambayo inawafanya watu wengi wasishiriki katika ubanguaji korosho hivyo kwa mwaka huu wamekuja na Teknolojia mpya ambayo inaendeshwa na umeme na kuondokana na ubanguaji wa korosho Moja moja kama ilivyokuwa hapo awali.
“Hii ni mashine ambayo wanavikundi au mwananchi mmojammoja wakiitumia inaweza kuwaingiza katika uanzishwaji wa viwanda vya ubanguaji wa korosho”
More Stories
TASHICO,yatoa ufafanuzi Mv.Serengeti kutitia upande mmoja
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua