Na Mwandishi wetu
Wahitimu wa mafunzo ya umahili katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) wametakiwa kuhakikisha ujuzi walioupata unawanufaisha watanzania .
Ameyasema hayo jijini Dar es Salaam jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka (UDART), Gilliard Ngewe wakati wa kongamano la 10 la Wahitimu wa Chuo NIT lililokwenda sambamba na utoaji wa zawadi kwa wahitimu waliofanya vizuri kwenye vitivo mbalimbali vya chuo hicho.
Amesema wahitimu hao wamepatiwa ujuzi wa kutosha hivyo ni wakati wao kwenda kutumikia jamii kwa kuhakikiha sekta ya usafirishaji inakuwa salama na yenye kuwanufaisha watanzania wote kwa ujumla
Kwa Upande wake Kaimu Mkuu wa chuo cha NIT Zainabu Mshana amesema Chuo chao kinajivunia kutoa wataalam wengi ambao wataokwenda kutoa suluhisho la usafiri nchini.
Amesema kuwa wanafunzi hao watakuwa chachu ya maendeleo kwa kuwa sekta hiyo ndio msingi wa maendeleo hapa nchini.
More Stories
Wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi watakiwa kusimamia programu za chakula shuleni
Mbowe akuna wengi kuhusu maridhiano
Waziri Chana amuapisha Kamishna uhifadhi NCAA, ampa maagizo mazito