December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wahasibu taasisi za elimu, afya watakiwa kuhakikisha ukataji kodi za zuio kwa wafanyabishara

Na Queen Lema, TimesMajira Online Arusha

Wahasibu kutoka katika taasisi za elimu pamoja na afya wametakiwa kuhakikisha kuwa wanasimamia ukataji wa Kodi za zuio kwa wafanyabiashara ambao wamepata zabuni ili kuweza kuruhusu serikali kuendelea kupata mapato yake.

Aidha kwa Sasa bado wapo baadhi ya wazabuni mbalimbali ambao hapo awali walikuwa hawaelewi umuhimu wa Kodi zuio Jambo ambapo kwa Sasa Kila mfanyabiashara katika sekta za elimu pamoja na afya wanatakiwa sasa kuhakikisha kuwa Kodi zuio zinakatwa kwa kuwa Kodi ni muhimu kwa ustawi wa taifa.

Hayo yameelezwa na Methew Dismas ambaye ni Meneja msaidi wa madeni kutoka katika mamlaka ya mapato mkoa wa Arusha(TRA) wakati akiongea na wadau wa shule pamoja na sekta ya afya na wahasibu kutoka Jiji la Arusha mapema hapo Jana Dismas alisema hapo awali wahasibu ambao ndio wasimamizi wa shuguli mbalimbali za kifedha bado baadhi Yao walikuwa hawajaweza kujua kuwa kuna umuhimu mkubwa Sana wa kukata Kodi hiyo ya zuio kutoka kwa wazabuni ambao wamepata fursa ya kupeleka au kusambaza huduma mbalimbali Katika sehemu zao za kazi.

“Hii Kodi ni muhimu Sana kwa maslahi ya taifa na pia Hii Kodi inatakiwa isimamiwe ipasavyo kwenye hizi idara kwa kuwa ni sehemu ya mapato ya Kodi na kama tujuavyo tusipolipa Kodi basi tutakuwa tunavunja na kuharibu sheria na kanuni za nchi kwa mujibu wa sheria”aliongeza.

Alisema kuwa mbali na kuwapa elimu hiyo pia wamefanikiwa kuwapa mbinu mbalimbali pamoja na kuwapa maelekezo staiki kwa mujibu wa sheria kama vile ambavyo inaelekeza kwa kuwa Kodi ni uhai wa taifa.

Naye muhasibu wa mishahara kutoka jiji La Arusha Bi Beatrice Mallya alisema kuwa Kodi za za zuio zinatakiwa kukatwa mara Tu baada ya huduma kufanyika.

“Kodi hizi zipo mara mbili na zinatakiwa kukatwa bila kumuonea mzabuni,kodi ya zuio na watoa huduma ambapo Kodi ya zuio inatakiwa ikatwe kwa asilimia 2 wakati Kodi ya kutoa huduma inatakiwa ikatwe kwa asilimia 5 pekee”aliongeza.

Alihitimisha kwa kusema kuwa Jiji Hilo limewapa elimu hiyo wadau hao ili kuweza kuwasaidia kujua Makato hayo ya zuio mara Tu baada ya huduma kufanyika ndani ya shule pamoja na hospitali mbalimbali.