November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wahasibu ni nguzo ya uchumi – Waziri Jamal

Na Mwandishi wetu, Timesmajira Online DSM

WAZIRI wa nchi Afisi ya Rais Ikulu – Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar CPA Jamal Kassim Ali amewataka wahasibu na wakaguzi wa hesabu kujua kuwa wao ni watu muhimu nchini katika kukuza uchumi na uimara wa Sekta ya fedha.

Ameyasema hayo Waziri wa nchi Afisi ya Rais Ikulu – Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar CPA Jamal Kassim Ali wakati wa ghafla utoaji wa Tuzo za Bodi ya wahasibu na wakaguzi wa hesabu Tanzania NBAA Jijini Dar es Salaam.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) CPA Prof. Sylvia Temu ameipongeza mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kuwa kinara wa uandaji mahiri wa Bora wa juu sana wa hesabu kwa Taasisi za serikali kwa kuzingatia viwango vya kimataifa kwa uwazi na kuwa miongoni mwa Mashirika yenye mipango endelevu yenye kuzingatia misingi ya Utawala bora.

Kwa upande wake Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, Alphayo Kidata amesema kwamba menejimenti yake itaendelea kusimamia kwa weledi na uadilifu katika ukusanyaji wa kodi za Watanzania.

Hivyo, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeibuka kinara kwenye tuzo zinazotolewa na Bodi ya Uhasibu na ukaguzi wa hesabu Tanzania Katika usiku wa utoaji tuzo desemba 01, 2023, TRA imepata tuzo mbili ikiwa ni pamoja na tuzo ya mshindi wa jumla, na tuzo ya mshindi wa kwanza kwa mashirika ya umma. Tuzo hizi zimezingatia viwango vya utunzaji wa mahesabu vya kimataifa (IPSAS).