July 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wahasibu ni nguzo ya maendeleo na uwekezaji

BODI ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) imesema kuwa hairuhusiwi mtu yeyote kufanya kazi za kihasibu bila kusajiliwa na Bodi hiyo na kuwa na CPA.

Hayo yamesemwa na Afisa Uhusiano na Mawasiliano wa NBAA, Magreth Kageya wakati akizungumza na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam katika maonyesho ya 48 ya biashara ya kimataifa sabasaba.

“Kuna watu wengi wanasema wao ni wahasibu, lakini kisheria mhasibu ni yule ambaye amesajiliwa mwenye CPA, kama Si mhasibu na kama hujapata CPA wewe siyo mhasibu bali unakua ni msimamizi wa Mhasibu, hivyo ili utambulike kisheria lazima uwe na CPA”

Amesema Waasibu wanamchango mkubwa kwenye maendeleo ya nchi yetu, kwani wanasaidia kutengeneza hesabu za fedha ambazo zinaenda kutumika kwenye maeneo mbalimbali mfano, uwekezaji

“Mtu ili awekeze anahitaji hesabu za fedha, ajue kuna faida gani na hasara gani pale atakapoenda kuwekeza”

Pia amesema wahasibu wanatumika kwenye kutengeneza Bajeti ya nchi

“Wao wanamchango mkubwa sana kukusanya maoni, kujua hiki kitatumikaje kwenye Bajeti yetu”

Aidha Kageya amesema wahasibu ni watu muhimu ambao wanasimamia rasilimali fedha kwa kuhakikisha fedha za Taasisi au kampuni zinatumika kiusahihi kwaajili ya kuleta maendeleo kwa mtu binafsi na kwa serikali kwa ujumla

Hivyo, Kageya amesema wahasibu wanapata faida nyingi ikiwemo mbali na kuajiliwa anaweza kujiajiri mwenyewe.