Na Mwandishi Wetu, Timesmajiraonline, Nachingwea
MADAKTARI Bingwa wa Dkt. Samia Suluhu Hassan, watatoa huduma ya matibabu kwa zaidi ya wagonjwa 6 0 0 wenye magonjwa
mbalimbali katika wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi kwa
siku siku.
Akizungumza wakati uzinduzi wa mpango huo, Wkuu wa Wilaya
ya Nachingwea, Mohamed Hassan Moyo, amewataka wananchi kutumia vizuri nafasi hiyo kupata huduma za kibingwa.
Moyo aliwaomba wananchi kuwafikishia taarifa wananchi
wengine ambao wanahitaji matibabu ya kibingwa katika
Wilaya ya Nachingwea kutoka kwa madaktari bingwa wa Dkt.
Samia.
Jumla ya madaktari bingwa sita wamewasili Wilaya ya
Nachingwea kwa ajili kutoa huduma mbalimbali kwa wagonjwa.
Huduma zitakazotolewa ni pamoja na huduma za upasuaji, ganzi
na usingizi, matibabu ya ngozi, huduma za afya kwa watoto, magonjwa ya ndani na magonjwa ya wanawake na
uzazi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea, Chionda Kawawa alimshukuru Rais Dkt. Samia suluhu Hassan kwa kuwapeleka madaktari bingwa katika Halmashauri
hiyo.
Mhandisi Kawawa alisema wananchi wanapaswa kuitumia vizuri fursa ya uwepo wa madaktari bingwa katika Halmashauri ya Nachingwea.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba