Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
WAGOMBEA wa CCM katika Uchaguzi wa chama Cha Mapinduzi wasiolipia kadi za mfumo wa Kielectronik majina yao KUKATWA .
Hayo yalisemwa na Mwenezi wa CCM mkoa Dar es Salaam Simon Mwakifamba, katika ziara ya mkoa Kata ya Buyuni katika mkutano ulioandaliwa na Diwani wa BUYUNI Athumani Maembe kutoa elimu ya Sensa na makazi kwa wanachama wake pamoja na kuwamasisha wanachama wa CCM wajiunge kwenye kadi za CCM za kisasa zilizo Katika mfumo Pamoja na kulipa ada.
Mwakifamba alisema Chama Cha Mapinduzi mkoa Dar es Salaam kinafanya ziara endelevu kwa wanachama wake kuwapa elimu ya Sensa KUHESABIWA pamoja na kuwataka wajisajili kadi za CCM katika mfumo wa kielectronik kila mmoja .
“Viongozi wa chama Cha Mapinduzi CCM mkoa Dar es Salaam tumeanza ziara endelevu ya utoaji elimu na kuwamasisha kujisajili pamoja na kulipa ada mfumo wa kisasa kielectronik kabla UCHAGUZI ndani ya chama tumejigawa katika ziara hii viongozi wote kutoa elimu Wagombea katika Uchaguzi huu wa chama kama hawajalipa kadi katika mfumo hawatoshi kuchaguliwa kuwa viongozi majina yao KUKATWA “alisema Mwakifamba.
Mwakifamba alisema CCM mkoa huo kina hamasisha wanachama wake kujiunga katika mfumo wa kisasa kielectronik kadi zao huku walipe ada ili wawe na sifa kwenye chaguzi mbalimbali za chama cha Mapinduzi.
Alitoa agizo kwa makatibu kata wote wakipokea vitamburisho vya CCM vya kadi za mfumo wa kielectronik kuziandika majina alafu kuzisambaza katika matawi yao Kila mmoja kuchukua tawini kwake.
Akizungumzia Uchaguzi wa chama Cha Mapinduzi CCM alisema Uchaguzi unafanyika Kila baada
miaka mitano, DHUMUNI la Uchaguzi wa chama kuchagua Wagombea wazuri watakaowezesha kupeperusha Bendera ya chama 2024/2025 Ili chama kiweze kushika dola.
Akizungumzia Uchaguzi wa chama Cha Mapinduzi unaotarajia kuanza hivi karibuni alisema mchujo utafanyika majina matatu ndio yatarudi yatapigiwa kura na wanachama.
Kwa upande wake Mwenezi wa CCM Wilaya ya Ilala SAID SIDDE aliwamasisha wanachama wa Wilaya Ilala pamoja na makatibu tawi pamoja na kata kutekeza maagizo yaliotolewa ikiwemo kuwamasisha Wana chama wa CCM wote kuingia kwenye mfumo wa kielectronik kwa wakati Ili wasipoteze haki ya kupiga kura.
DIWANI wa Kata ya Buyuni Athumani Maembe aliwataka wanachama wake wa CCM Kata ya Buyuni kujisajili Katika mfumo wa kadi ya kisasa Ili wasipoteze haki yao.
Diwani Athumani Maembe aliwataka wanachama wa chama Cha Mapinduzi CCM waache kuishi kwa mazoea badala yake wapende Chama Cha Mapinduzi CCM na Jumuiya zake.
More Stories
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu