January 15, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wafanyabishara watakiwa kuwa na uadilifu

Na Penina Malundo, timesmajira , Online

WAFANYABIASHARA wametakiwa kufanya biashara kwa uadilifu kwenye kazi wanazozizalisha ili kutengeneza imani kwa wateja wao.

Rai hiyo imetolewa leo na Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dk. Ashatu Kijaji wakati wa maadhimisho ya miaka 15 ya utendaji kazi wa Kampuni ya GF Truck and Equipment Ltd yaliyofanyika ndani ya maonesho ya 46 ya kimataifa ya biashara yanayoendelea katika uwanja wa Mwalimu Nyerere. 

Kijaji amesema wateja wengi wamekuwa na malalamiko ya kupokea bidhaa tofauti na ile walioagiza hivyo anawataka wafanyabiashara wakiwemo wa mitandaoni kujenga imani kwa kutoa bidhaa halisi.

Mkurugeni wa kampuni ya Gf Truks,Imran Karmal akimkabidhi zawadi Waziri wa Viwanda na uwekezaji Ashatu Kijaji katika viwanja vya maonesho leo.

“GF Truck and Equipment Ltd wanafanya kazi nzuri sana kwani magari wanayounganisha yana ubora na viwango vinavyokubalika na wateja wao wamekuwa wakipokea bidhaa zilizobora,” amesema

Hata hivyo Waziri Kijaji ameipongeza Kampuni ya GF Truck and Equipment Ltd kwa namna wanavyofanya kazi ya uunganishaji magari kwa viwango bora vinavyokubalika kimataifa.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa GF Truck and Equipment Ltd, Imran Karmal amesema hadi kufikia jana wamefanikiwa kuunganisha gari la 600 na wamekuwa wakitoa ajira kwa vijana wa kitanzania.

“Malengo yetu ni kuendelea kuunganisha magari mengi zaidi kwa viwango na vigezo vya kimataifa, magari yetu yanaungwa na vijana wa kitanzania,” amesemaÂ