November 22, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wafanyabiashara watakiwa kuwa makini na vifungashio

Meneja wa wakala wa vipimo (WMA) mkoa wa kinondoni  bi Lilian  Mombeki akionyesha miongoni mwa bidhaa walizozikamata ikiwemo gundi ya malumalu (grout) ambavyo ilikuwa na ujazo pungufu kwenye kifungashio.

Na Bakari Lulela, Timesmajira Online DSM

WAKALA wa vipimo (WMA) mkoa wa kinondoni jijini Dar es Salaam wamewataka wafanyabiashara kuwa makini na vifungashio ambavyo ni halali kwa ujazo wa bidhaa wanazozitoa,

Hayo yameelezwa na Meneja Lilian Mombeki alipokuwa na mahijiano na chanzo hiki amesema wamekua na zoezi la kustukiza kwa wafanyabiashara mbalimbali.

“Mara nyingi huendesha zoezi la ukaguzi wa kustukiza kwa wafanyabiashara mbalimbali ambapo kwa watakaobainika wakiendesha biashata hizo kinyume na utaratibu huchukiliwa hatua kwa mujibu wa Sheria,”amesema Lilian

Aidha Lilian ameeleza na kuonyesha baadhi ya bidhaa walikuwa wamezikamata kwa wateja ambapo si waadilifu kama vile gundi ya malumalu grout ambavyo ilionekana kupunjwa ujazo ndani ya kifungashio.

Aliongeza kwa kusema vipimo vyote vinavyotarajia kutumika katika sekta ya biashara, afya, mazingira na usalama haviruhusiwi kutumika kabla ya kuahakikiwa na wakala wa vipimo.

Mamlaka hiyo wamekwa wakifanya uhakiki wa pampu kila mwaka kulingana na ratiba na baada ya uhakiki wanaendelea na ukaguzi wa kustukiza kila ktuo cha mafuta klichopo eneo la kinondoni.

Meneja huyo amesema huanza ukaguzi kwa mzalishaji mkuu wa bidhaa halafu huendelea kwa kushuka kwa wazalishaji wadogo.

Wito umetolewa na wakala hao mtu yeyote atakae onekana  akifanya biashara kinyume na utaratibu wa serikali atachukuliwa hatua ikiwemo kulipa faini hivyo wananchi wametalkiwa kutoa taarifa kwa wakala wa vipimo.