Na Penina Malundo,TimesMajira,Online
WANAWAKE wanaofanya shughuli zao sokoni na wanauza mbogamboga na Matunda wametakiwa kufichua vitendo vya ukatili wa kijinsia vinavyotoka katika jamii zao zinazowazunguka hususani ndani ya kaya zao.
Akizungumza hayo jana jijini Dar es Salaam Mtaalamu wa masuala ya Jinsia ,ChristinaWarioba ,amesema licha ya wamama hao kufanya shughuli zao za kila siku za biashara lakini wanapaswa kuangalia familia wanazoziacha majumbani mwao kabla na baada ya kurudi nyumbani.
Amesema ni vema kukaa na watoto wao na kuongea nao juu ya masuala ya ukatili wa kijinsia na sio kuwaacha watoto na kuangalia biashara zao.
“Ukatili wa kijinsia bado upo na unafanya na watu wa karibu tunapaswa wamama wa masokoni kufanya mabadiliko kwani ukatili wa ngono unafanywa majumbani kwetu,”amesema na kuongeza
“Katika siku 16 za ukatili wa kijinsia inapaswa kuangalia na kuwafikia watu wa makundi yote ili elimu hii iwafikie na waje ni namna gani ukatili wa kijinsia unavyofanyika hususani kwa watoto ambao wao wanahatari pindi wanapoenda shule wanafanyiwa ukatili wa kingono njiani na anashindwa kusema,”amesema
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya Women Tapo Tanzania ambaye pia Mkurugenzi wa Taasisi ya Tabata Women Tapo,Stella Mbaga amesema taasisi yao inafanya kazi na wamama wa masokoni na inawasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuwapa elimu mbalimbali ikiwemo ya afya hasa katika Kansa na Uzazi,Masuala ya Kiuchumi katika kuwaunganisha na taasisi mbalimbali za kifedha pamoja na elimu za jamii hususani za ukatili wa kijinsia.
Amesema ukatili wakingono kwa wamama wa masokoni unafanyika sana na wanapaswa wamama hao kulewa elimu kwani unakuta mama anaenda sokoni kufanya shughuli zao huku nyuma ndugu au Baba aliyemuacha nyumbani anafanya ukatili kwa watoto waliopo nyumbani.
Naye Mmoja wa Waathirika wa Masuala ya Ukatili wa Kijinsia ,Hellen Daniel amesema hadi sasa amekuwa muathirika mkubwa wa ukatili wa kijinsia kutokana na maisha anayoyapitia ambapo ametelekezwa na Mtoto Mlemavu mwenye umri wa miaka 4 huku kwenye nyumba aliyopanga anatakiwa kuondoka kutokana na kushindwa kulipa kodi.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa