Na Mwandshi Wetu, TimesMajira Online, Dodoma
WAFANYABIASHARA Jijini Dodoma waikubali huduma ya LIPA KWA SIMU inayotolewa na Mtandao nambari Moja unaoongoza kwa mapinduzi ya Kidigitali Tigo Tanzania, ambapo sasa Tigo inatoa ofa na Promosheni mbalimbali za kusisimua kwa wateja wake hasa kuelekea Serengeti Music Festival 2022.
Akithibitisha hilo , Meneja wa Huduma za Malipo Tigo – Pesa Reuben Kamuga amesema kuwa Tigo wanatambua umuhimu wa kuenzi tamaduni za kitanzania, kukuza tasnia za muziki nchini, kukuza vipaji vya wasanii wachanga , kuibua fursa za kibiashara , na kutoa elimu ya ujasiriamali katika maeneo mbalimbali nchini .
“Kuendana na shangwe la Serengeti Music Festival 2022 kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya Kidigitali hapa nchini Tigo inatoa huduma, Ofa na Promosheni mbalimbali za kusisimua.
Kupitia huduma ya LIPA KWA SIMU kwa kushirikiana na bar mbalimbali hapa Dodoma.
Dunia Sasa hivi Ipo kiganjani kupitia simu ya mkononi sasa unafanya Malipo popote ukiwa na huduma ya LIPA KWA SIMU ambapo kwenye tamasha hili la Serengeti Music Festival 2022 wateja wa Tigo wataweza kulipia vinywaji na vyakula Kidigitali huku wakiendelea kupata burudani.
Tunawakaribisha wateja wetu kufurahia Ofa hizi kutoka Tigo lakini pia kujumuika nasi katika viwanja vya Chinangali weekend hii ili tuweze kujumuika pamoja” alisema bwana Kamuga
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Chanangali Park Frank Ngonyani amewakaribisha wakazi wa Dodoma kutembelea viwanja ivyo kwa ajili ya Kushuhudia Serengeti Music Festival 2022 ambapo mdau mkubwa katika Tamasha Hilo ni Tigo Pesa , Aidha amewapongeza kwa kuendelea kuwa wabunifu na kutoa huduma za Kidigitali kwa wateja wake.
More Stories
TASHICO,yatoa ufafanuzi Mv.Serengeti kutitia upande mmoja
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua