Na Penina Malundo,timesmajira, Online
MIKOKO ni miongoni mwa miti ambayo inaoota ufukweni mwa bahari na kwenye mito ambayo inasaidia kuimarisha uhakika wa chakula, kuendeleza uvuvi na bidhaa zingine za msituni ikiwemo ufugaji wa nyuki na mazao yake. Pia inaumuhimu wa kipekee wa kukusanya na kuhifadhi kiasi kikubwa cha gesi ya ukaa kutoka hewani na baharini,ambacho ni muhimu kwa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Kila ifikapo Julai 26,kila mwaka mataifa mbalimbali yanaadhimisha siku ya mikoko duniani,huku wadau wakitoa wito juu ya umuhimu wa miti hiyo katika nchi na duniani kote. Katika kuadhimisha siku hiyo Taasisi mbalimbali za mazingira ikiwemo Taasisi ya Hudefo, Taasisi ya Point of coreection Environment Tourism and Entertainment (ETE),Taasisi ya Mazingira Plus, pamoja na taasisi ya Tanzania clean up and conservation Initiative ( TCCi), zimeweza kushirikiana na kufanya maadhimisho hayo Wilayani Mkuranga mkoani Pwani,Kijiji cha Mdimni Kata ya Magawa.
Sara Pima ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Hudefo,anasema katika utunzaji wa mazingira ni vema jamii kuhakikisha inatunza mikoko ambayo inafaida nyingi duniani. Anasema mabadiliko ya tabianchi ni miongoni mwa changamoto inayojitokeza katika kufanya uharibufu katika miti hiyo hivyo kuna umuhimu wa vijiji vinavyozunguka pwani ya bahari kuhakikisha inapanda mikoko na kuitunza vizuri ili iweze kuwaletea tija katika vijiji vyao. Pima anasema katika kijiji cha Mdimni tayari mabadiliko hayo yameanza kuonekana na baadhi ya maeneo ya mikoko yameweza kuathiriwa na kusababisha kupotea kwa mikoko mingi. “Sisi kama muungano wa taasisi nne,tumeamua kwa dhati kufanya kazi na kijiji hiki mdimnu katika mradi wa mikoko,tumefanya hivi baada ya kuona mabadiliko ya tabianchini yalivyoweza kuathiri kijiji hicho ambapo wanatoa elimu juu ya utunzaji wa mazingira na ulindaji wa mikoko hiyo ambayo inafaida kubwa katika maeneo yao na nchi kwa ujumla,”anasema na kuongeza ”Katika kuhakikisha Miti hiyo inatunzwa ipasavyo,tumekuwa na vikundi vya wakinamama vinavyojishughulisha na Shughuli za ufugaji wa Nyuki, katika maeneo hayo ya mikoko hivyo tumeweza kuwajengea uwezo katika umuhimu wa utunzaji wa mikoko kwa kushirikiana na Wakala wa Misitu nchini TFS,”anasema. Pima anasema hadi sasa wakinamama hao wanavikundi 12 kati ya hivyo vikundi Vinne vimesajiliwa huku vingine vinaendelea na utaratibu wa usajili ambapo kila kikundi kina watu 40 na wanajihusisha na masuala ya ujasiliamari, kama Nyuki ,Ufugaji ,Uvuvi pamoja na Kilimo . Anasema katika kuadhimisha siku hiyo ya mikoko wameweza kuwasaidia wanavikundi wa kijiji hicho mizinga minne ya nyuki ambayo itawasaidia katika shuguli zao za ufugaji wa nyuki katika mikoko hiyo huku wakiendelea kuilinda ipasavyo. ”Mbali na mizinga hiyo pia tunatarajia kupokea mizinga mingine 15 kutoka kwa TFS ambayo nayo tutawaletea wanavikundi hawa ambayo itaendelea kuwasaidia katika shughuli zaoi hizo,”anasema.
Anasema katika kuadhimisha siku hiyo ya mikoko wameweza kuwasaidia wanavikundi wa kijiji hicho mizinga minne ya nyuki ambayo itawasaidia katika shuguli zao za ufugaji wa nyuki katika mikoko hiyo huku wakiendelea kuilinda ipasavyo. ”Mbali na mizinga hiyo pia tunatarajia kupokea mizinga mingine 15 kutoka kwa TFS ambayo nayo tutawaletea wanavikundi hawa ambayo itaendelea kuwasaidia katika shughuli zaoi hizo,”anasema. Anasema katika maadhimisho hayo pia wameweza kupata mito ya mikoko 250 katika kijiji hicho kwa lengo la kuendelea kuotesha miti hiyo inayosaidia katika shughuli zao mbalimbali. ”Tunashukuru kwa kushirikiana na wadau kwa kuungana katika kulinda misitu yetu na vyanzo vya maji na mikoko ili kuweza kutimiza malengo ya maendeleo endelevu,”anasema na kuongeza. “Tunamshukuru Raisa Samia Suluhu Hassan kwa kutia mkazo na kushirikisha wadau mbalimbali wa maendeleo katika kusisitiza uchumi wa Blue,tunaamini mikoko ni sehemu inayochangiza uchumi wa Blue katika sekta mbalimbali ikiwemo utalii na uvuvi hivyo kama wadau wa mazingira tunaunga mkono jitihada za Rais Samia katika kuhakiakisha tunashiriki katika uchumi wa blue,”anasisitiza
Kwa Upande wake Msemaji waTaasisi ya Tanzania Clean Up and Conservation Initiative (TCCi),Innocent Mahendeka anasema wameenda kuadhimisha siku hiyo ya mikoko ikiwa ni sehemu ya utaratibu wao wa mwaka wa tatu katika kuadhimisha siku hiyo duniani.
Anasema sababu kubwa ya kuadhimisha katika kijiji hicho cha Mdmni ni kutokana na kuwa sehemu ya mfano wa vijiji ambavyo vimeliwa na mabadiliko ya tabianchi.
”sisi kama taasisi wadau wa mazingira tumefanya tafiti na kufika katika eneo hili na kuona athari kubwa iliyowakuta wakazi wa eneo hili kijiji chao kuingia katika athari ambacho baadae ingwaletea tatizo katika uchumi wao,”anasema na kuongeza ”Waliona kuna haja ya kutoa elimu na kufanya utekelezaji wa kudhibiti hali hiyo,leo tumeshirikiana na wadau wengine katika kuendelea kutoa elimu na kuwapatia misaada mbalimbali ya mizinga ya nyuki kwaajili ya ufugaji,”anasema.
Anasema serikali iendelee kuunga mkono jitihada zinazofanya na wadau wa mazingira ambao wanaangaika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ili kipindi kijacho waweze kuokoa walau sehemu ya maisha ya watu na dunia ili shughuli za kiuchumi na kujipatia kipato iweze kuendelea.
Naye Afisa Mradi na Mshauri elekezi katika Mabadiliko ya Tabianchi kutoka Shirika la ForumCC,Baraka Machumu anasema katika kijiji hicho kilikuwa na zaidi ya hekari 1500 ambapo kati ya hekari… ziliweza kuharibika. Anasema Mikoko inafaida ya kupunguza joto,kusafisha bahari na kuzuia kwa kumomonyoka maeneo ya nchi zilizopo kando ya bahari.
”tunapoelekea katika mkataba wa Paris kama wadau tunajukumu la kupunguza joto na hata katika makubaliano mbalimbali kunamikakati ambayo inatuambia tupunguze uzalishaji wa gesi joto huku mikoko ni moja ya mimea inatoa michango mikubwa ya kupunguza gesi joto duniani na kuleta mvua katika maeneo ya kanda ya bahari ya hindi,”anasema
”Utunzaji wa mikoko inafaida kubwa katika kukabiliana na kuhimili katika mabadiliko ya tabianchi katika maeneo mbalimbali nchini,”anasema Abdallah Mikulu Mkurugenzi wa Taasisi ya Mazingira Plus anasema kuna umuhimu mkubwa wa Mikoko duniani kwani ni moja ya ikolojia bora zaidi katika kufyoza hewa ya ukaa na ni mara tano ya misitu ya kawaida. Anasema pia Mikoko inapatikana katika maeneo ambayo yanakutana kati ya mto na bahari na hayo maeneo ni muhimu katika mazalia ya ikolojia mbalimbali za baharini ikiwemo samaki na viumbe vingine vya bahari kama kama,kaa na wadudu wengine. “Mikoko inatumika katika kuzuia yale mawimbi makali ya bahari kuingia katika sehemu ya ardhi na maeneo mengi yaliyoathirika yanapata kuingia moja kwa moja kuathiri,”anasema na kuongeza “Kutokana na mabadiliko ya tabianchi kina cha maji cha bahari yameongezeka na kupelekea maji kuongeza na kusababisha uharibifu wa Beach na maji kuingia sehemu za nchi kavu na kwend kuathiri vyanzo athari vya maji,”anasema.
More Stories
Mbowe akuna wengi kuhusu maridhiano
Waziri Chana amuapisha Kamishna uhifadhi NCAA, ampa maagizo mazito
Amos Lengael Nnko afariki kwa ajali ya gari