November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wadau wa maendeleo watakiwa kusaidia serikali kutatua changamoto za wananchi

Na Hadija Bagasha, TimesMajira Online, Tanga

Wadau wa maendeleo na taasisi mbalimbali zisizokuwa za kiserikali zimetakiwa kuisaidia serikali katika kutatua changamoto zinazowakabili wananchi kabla ya serikali kuchukua hatua.

Hayo yamesemwa na Msemaji wa taasisi ya The desk and chair foundation kanda ya kaskazini Mzamil Yusuf wakati akikabidhi visima vitatu vya maji katika eneo la Mabawa, Mnyanjani na Masiwani vilivyogharimu zaidi ya milioni 45.

Awali akizungumza wakati akikabidhi visima hivyo msemaji huyo amesema kuwa wao kama wadau wa maendeleo wameona wasisubiri tu serikali itatue changamoto za wananchi bali taasisi zinapaswa kuguswa kwa kuona wananchi wana uhitaji wa jambo gani.

“The desk & chair foundation imekuwa ikiisaidia serikali katika suala la mahitaji ya madarasa kwa shule za msingi na sekondari inasaidia madawati, lakini vilevile inajenga vyoo vya kisasa kabisa kwa shule za msingi na sekondari lakini vilevele tunajenga vyoo katika vituo vua, huduma za afya ikiwa ni pamoja na kusaidia vifaa tiba, “alisistiza Msemaji huyo.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa visima hivyo Mwenyekiti wa Taasisi ya Shia Ithna Asher Jamaat Mkoa wa Tanga Hussein Warj ameshukuru kwa msaada huo wa kujengewa visima hivyo ambavyo vinakwenda kuwasaidia wanatanga.

Alisema visima hivyo vinakwenda kuondoa adha ya majo kwani kata hizo zilikuwa zikikabiliwa na shida ya maji ambapo hivi sasa wanapata maji safi na salama.

“Kina mama walikuwa wakienda masafa marefu kufuata huduma hiyo ya maji tena kwenye visima vya mitaani ambavyo maji yake sio safi na salama kwa afya zao lakini kwa sasa wanapata maji safi karibu kabisa na maeneo yao isitoshe maji haya haya yatakuwa yakitumika hata misikitini hivyo imesaidia sana, “alisistiza Hussein.

Alitoa shukrani kwa wadhamini wa msaada na kuwaomba waendeles kusaidia huduma hiyo kwani uhitaji wa maji katika mkoa huo bado ni mkubwa hivyo waendeleze msaada hup ili kina mama waomdokewe na adha ya kufuata maji umbali mrefu.

Baadhi ya kina mama waliokuwepo katika moja ya visima vilivyojengwa akiwemo Kuruthumu Ally mkazi wa, Donge alisema hapo awali walikuwa wakikabiliwa na changamoto ya ukosefu wa maji ambapo walikuwa wakisubiria maji ya mvua katika visima jambo ambalo wakati wa kiangazi limekuwa likiwapa wakati mgumu kutokana na visima hivyo kukauka.

“Tulikuwa tunatumia muda mrefu kutafuta maji ilikuwa tunatoka asubuhi saa 11 mpaka saa sita mchana ndio unapata ndoo moja au mbili ya maji hata kina baba wanaona namna tunavyohangaika, “alisema Kuruthumu.

Pamoja na uwepo wa maji Toka mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira (Tanga Uwasa) wakati mwingine adha hutokea dharura na kukosekana maji hivyo visima hivyo vitasaidia katika Hali Kama hiyo inapojitokeza

Zaidi ya visima vya maji 25 tayari vimeshajengwa Mkoani Tanga ambapo kwa Tanzania nzima mpaka sasa Taasisi hiyo isiyo ya kiserikali ya The desk and chair foundation yenye makao yake makuu jijini Mwanza imeshajenga zaidi ya visima 600 ambapo mwenyekiti wa Taasisi hiyo ni Siptain Merji.

Visima hivyo vimekabidhiwa kwa Taasisi ya Shia Jamaat Tanga kwa ajili ya usimamizi na uangalizi ikiwemo kuvihudumia katika dharura ya kiufundi na umeme (Luku) ili jamii iendelee kupata huduma ya maji kwa wakat wote na Bila ubaguzi wa rangi,dini,chama au kabila.

Msaada Huo kupitia the desk & Chair foundation umetolewa na washirika wa karibu wa taasisi hiyo kama sadaka na kumbukumbu kwa wazazi wao walitangulia mbele ya Haki.