January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wadau wa maendeleo waombwa kujitokeza kusaidia ujenzi Sekondari Musoma Vijijini

Fresha Kinasa,TimesMajira Online,Mara.

WADAU mbalimbali wa Maendeleo na Wazaliwa wa kata za Etaro,Ifulifu na Bugwema katika Jimbo la Musoma Vijijini  Mkoani Mara wameombwa  kujitokeza  kusaidia ujenzi wa Shule za Sekondari zinazojengwa kwa nguvu za  wanananchi  katika kata hizo  na  mwakani  2025 zitafunguliwa. 

Hayo yamebainishwa kupitia taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Disemba 18, 2024. Ambapo imeeleza kuwa, Sekondari  zinazojengwa kwa nguvu za Wananchi ni Muhoji Sekondari inayojengwa Kijijini Muhoji, Kata ya Bugwema. Imeanza kupokea fedha za kuchagia ujenzi kutoka Serikali Kuu (sekondari ya pili ya Kata)

Sekondari nyingine ni Rukuba Island Secondary School  Kisiwani Rukuba, Kata ya Etaro ambapo Kijiji cha Mmahare kinaanza kujenga sekondari yake (sekondari ya tatu ya Kata),  pia Nyasaungu Sekondari inayojengwa
Kijijini Nyasaungu, Kata ya Ifulifu ni
(Sekondari ya pili ya Kata)

“Michango inakaribishwa, Wanavijiji wanaojenga sekondari hizo tatu wanaendelea kuomba michango kutoka kwa wazaliwa wa maeneo hayo, na kutoka kwa Wadau wengine wa Maendeleo.” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa,  Sekondari zinazojengwa kwa fedha nyingi kutoka Serikali Kuu, na zitafunguliwa mwakani (2025). Wanavijiji wanachangia nguvukazi ni Butata Sekondari Kijijini Butata, Kata ya Bukima ambapo  Serikali imechangia Shilingi Mil. 584,(Sekondari ya pili ya Kata)

Pia, Sekondari ya amali/ufundi
Kijijini Kasoma, Kata ya Nyamrandirira
Serikali imechangia Shilingi Mil
584, ni (Sekondari ya tatu ya Kata),
Daud Massamba Memorial Secondary School  Kijijini Kurwaki, Kata ya Mugango. Ambapo Serikali imechangia Shilingi Mil.  584, (Sekondari ya pili ya Kata).

Upande wa Sekondari zilizokamilisha matayarisho ya kuanza ujenzi kwa kutumia nguvu za wananchi ni 6 ikiwa ni pamoja na  Chitare Sekondari, Kata ya Makojo (sekondari ya pili ya Kata), Sekondari Kijijini Nyambono,  (sekondari ya pili ya Kata,  Musanja Sekondari, Kata ya Musanja. (sekondari ya pili ya Kata).

Kataryo Sekondari, Kata ya Tegeruka (sekondari ya pili ya Kata), Mwigombe Tech Sec, Kijijini Kiriba (sekondari ya tatu ya Kata), Mmahare Sekondari, Kata ya Etaro  (sekondari ya tatu ya Kata). Na pia Wanavijiji wanaojenga sekondari hizo sita wanaomba michango kutoka kwa wazaliwa wa maeneo hayo, na kutoka kwa Wadau wengine wa Maendeleo.

Jimbo la Musoma Vijijini lina  Kata 21, zenye vijiji 68,  na vitongoji 374, ambapo idadi ya Sekondari Jimboni humo za kata ni 26, Sekondari Binafsi 2, Sekondari mpya 2025 ni 6, na Sekondari Mpya zinazoanza kujengwa ni 6. Huku idadi ya High school ni  pamoja na Kasoma, masomo ya “arts”, Suguti, masomo ya sayansi, 2025, na Mugango, masomo ya sayansi, 2025.

“Tunaendelea na ujenzi wa maabara tatu za masomo ya sayansi (physics, chemistry & biology) kwenye sekondari zetu zote ili tuongeze idadi ya “high schools” za masomo ya sayansi Jimboni mwetu.”imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Shadrack Paul ni Mkazi wa Kata ya Etaro akizungumza na Times Majira amesema kuwa Jimbo la Musoma Vijijini limeendelea  kuwekeza katika Sekta ya elimu. Huku akisisitiza kuwa Mbunge waJimbo hilo Prof. Muhongo ni Mpenda maendeleo, hivyo mkakati wake  ni kuhakikisha Jimbo lake linaandaa  Wasomi wengi kwa manufaa ya Jamii na Taifa kwa siku za usoni.