March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wadau wa Biashara watoa maoni yao kuelekea Jubilee ta miaka 50 ya Sabasaba

Na Mwandishi wetu,Timesmajira

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) kwa kushirikiana na taasisi za umma na binafsi pamoja na wadau wa biashara wamefanya tathmini ya Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam Sabasaba 2025 na kupanga makubwa kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya miaka 50 ya Sabasaba yanayotarajiwa kufanyika 28 Juni mpaka Julai 13, 2026.

Akibainisha Maonesho3, Dkt. Latifa Khamis – Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, amebainisha Maonesho yamechagiza makubwa katika uchumi wa nchi kwa kuongeza mzunguko wa fedha, upatikanaji wa fedha za kigeni, kufurika kwa wateja kwenye mahoteli na ongezeko la ajira za muda mfupi hususan kwa vijana na wakina mama.

Aidha Dkt. Latifa, amewakaribisha wadau mbalimbali wa biashara kutoa maoni kwa lengo la kuboresha na kuongeza ubunifu kwenye Maonesho ya Dhahabu ya Sabasaba miaka 50.


Tathmini hiyo imefanyika katika ukumbi wa Rashid Mfaume Kawawa (Ceremonial Dome) uliopo katika kiwanja cha Mwl. Julius Nyerere, Dar es Salaam.Move upMove downToggle panel: OneSignal Push NotificationsMove upMove downToggle panel: Yoast SEOOpen publish panel