November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mkurugenzi wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Hakirasilimali Bi Racheal Chagonja ameishauri serikali kitenga fedha kwa ajili kufanya tafiti zitakazowasaidia wachimbaji wadogo kunufaika na rasilimali za madini.

Wadau sekta ya madini waishauri Serikali kutenga fedha za tafiti

Na Bakari Lulela,TimesMajira Online, Dar

WADAU wa sekta ya madini nchini wameishauri serikali kutenga fedha kwa lengo la kufanya tafiti mbalimbali zitakazowawezesha wachimbaji wadogo kunufaika na rasilimali za madini.

Hayo yamebainishwa mkoani Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Hakirasilimali Racheal Chagonja ambapo amesema wachimbaji wadogo wamekuwa wakifanya shughuli za uchimbaji madini bila kunufaika ni bidhaa hiyo.

“Tasnia ya uchimbaji wa madini imekuwa ikitanuka siku hadi siku na kuzidi kuchochea uchumi wa nchi kuongezeka,lakini uchimbaji huo umekuwa na changamoto kwa wachimbaji wadogo kwa kukosa fedha na maarifa ya kutosha,” amesema Racheal.

Aidha Racheal amesisitiza uwepo wa mabadiliko ya sera na sheria zitakazo liwezesha kundi hilo kufanya kazi za uchimbaji kwa manufaa yao na nchi kwa ujumla sambamba na kuendeleza mijadala mbalimbali yenye tija kwa wadau hao.

Hata hivyo Rachael ameeleza kwamba wachimbaji hao wananafasi kubwa katika kuchangia pato la Taifa ili waweze kunufaika inahitajika kuwa na sera madhubuti zitakazosaidia wachimbaji hao kupata mafanikio.

Ameongeza kwa kusema uwepo wa elimu ya uchenjuaji wa bidhaa hiyo inahitajika kwenye kundi hilo sambamba na nidhamu ya matumizi ya fedha yatakayowanufaisha wao na familia zao.

Hakirasilimali imedai kwamba sekta ya madini eneo muhimu kwa maendeleo ya jamii na nchi kwa ujumla ambapo wamezitaka taasisi zinazohusika na masuala ya kodi ziweze kutoa uelewa kwa wadau hao ili waweze kulipa kodi kwa wakati.

Mwishooo