January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wachimbaji watakiwa kutumia vifaa vyenye ubora

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Ruangwa 

WACHIMBAJI wadogo wametakiwa kutumia vifaa vyenye ubora kuanzia kwenye uchimbaji hadi kwenye uchkataji wa madini kwa ajili ya maslahi mapana kwao wenyewe na Taifa kwa ujumla.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya vifaa vya ujenzi  SHEVA ‘ SHEVA HARDWARE’ MaryStella Temba wakati akizungumza na waandishi wa habari katika banda lao kwenye maonyesho ya madini yanayoendelea katika wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi.

“Sisi kama wauzaji wa vifaa vya uchimbaji madini tumekuwa kwenye tasnia hii kwa muda mrefu na tumegundua kuwa iko haja ya wachimbaji wadogo kutumia vifaa bora kutoka kwetu kwani vina ubora wa hali ya juu  na unaomuhakikishia muhuiska anayevitumia usalama wake.

Ametumia nafasi hiyo kuwakaribisha wananchi hasa wawekezaji wa madini kwenye banda lao ili waweze kujinea wenyewe lakini pia ikiwa ni pamoja na kupata vifaa mbalimbali vinavyorahisha shughuli zao.”amesema na kuongeza kuwa

“Hii ni  Kampuni ya kitanzania ambayo imejipambanua kuuza na kusambaza vifaa mbalimbali ikiwa pamoja na majembe,sululu, kofia ngumu, viatu ,Nondo,  na vinginevyo.”amesema Merystella 

Aidha amesema kampuni hiyo imejipanga vizuri  kuhakikisha wanatoa huduma Bora na sahihi kwa watanzania .

Mkurugenzi huyo amesema ,wameanza na mkoa wa Lindi kwa sababubu ni mkoa ambao unasemekana una madini ya aina nyingi hapa nchini kuliko mikoa yote kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa na tume ya madini.

Marystella ameongeza kuwa anawakaribisha wananchi wote kutembelea banda lao lililopo  ndani ya viwanja vya soko jipya  kilima hewa kujionea vifaa vya ujenzi vyenye ubora na kupata bei nafuu kuliko mahala pangine popote pale.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo ,kwa sasa kampuni yao inatoa huduma katika mikoa miwili ya Dar es Salaam na Lindi huku akiwataka wadau wote kutoka maeneo na mikoa mbalimbali kujiyokeza kwa wingi kwa ajili ya kupata ushauri.