Na Esther Macha,TimesOnline,Mbeya
WACHIMBAJI wadogo wa madini ya dhahabu halmashauri ya wilaya ya Chunya mkoani Mbeya wameiomba Serikali kuwawezesha kupata mikopo ili waweze kununua vifaa vya kisasa ikiwemo mashine za kuchenjua madini ili kuzuia upotevu wa madini .
Hayo yamesemwa leo,Agosti 3,2023 na Mkurugenzi Kampuni ya AGM inayojishughulisha na utengenezaji mitambo ya uchechuaji wa madini ya dhahabu ,Andrew Mpangwe wakati akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya Maonesho ya wakulima ya Nanenane vya John Mwakangale vilivyopo mkoani Mbeya.
Aidha Mpangwe amesema kuwa kwasasa wanahitaji fedha nyingi kwasababu ni kazi endelevu ambayo ni ngumu kuweka kiwango kwani tunaweza kuomba hata kuanzia mil.30 mpaka 200.
“Tunahitaji fedha nyingi kwani machimbo ya madini chunya ni mengi,kuweka kiwango huwezi maana unaweza kuweka mil.30 mpaka 200 maana tukipata mikopo inaweza kuwa msaada mkubwa kwetu”amesema
Ametoa sababu kutopata mkopo hadi sasa amesema ndo wanaanza kazi hiyo ya utengenezaji wa Makalasha ambapo mpaka sasa wana mwaka mmoja.
Hata hivyo Mpangwe ameshukuru halmashauri ya wilaya ya chunya kwa kuwapatia maeneo ya kufanyia kazi kwani imewasaidia na halmashauri kuwaunga mkono kufika kwenye maonesho kutangaza biashara hiyo.
Aidha amesema kuwa ana vijana 20 ambao amewaajiri na huku akiwataka vijana wengine zaidi kujitokeza katika utengenezaji wa Makalasha, uchimbaji na uhasibu.
Pamoja na hayo Mpangwe ametaja changamoto zinazowakabili huku akisisitiza upatikanaji wa mtaji kuwa ni changamoto kubwa pamoja na upatikanaji wa malighafi ambayo yanahitaji usafiri kuwa na vibali .
Vilevile, ameimba serikali kuwafikishia umeme kwenye maeneo ya migodi na mitambo ili kuondokana na gharama kubwa ya mafuta kwani umeme ni nafuu kwa maeneo ya migodi ambako kutachochea mapato ya serikali.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Chunya na Diwani wa kata ya Kiwanja,Bosco Mwanginde amekiri kutokukipatia kikundi cha uchimbaji mikopo kwani wakati halmashauri imejipanga kuwapatia, serikali ilisimamisha utoaji mikopo kwa vikundi mpaka watakapopatiwa maelekezo mengine .
“Vikundi vingine viendelee kujipanga wakati serikali ikifanya utaratibu mwingine lakini hichi kikundi pale utaratibu utakapokuwa tayari watakuwa kikundi cha kwanza kuwezeshwa kupata mikopo”amesema Mwenyekiti Mwanginde.
Mwanginde amesema tayari kuna mtambo wa usagaji mawe kwa ajili ya dhahabu na wanaonyesha jinsi ya kufanya kazi.
More Stories
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato