December 29, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Waandishi wapatiwa mafunzo ya uandishi wa kisayansi

Na Angela Mazula,TimesMajira. Online

WAANDISHI wa habari jijini Dodoma, wamepatiwa mafunzo ya uandishi za kisayansi kuwajengea uwezo wa kufikisha taarifa sahihi kwa jamii wakiwemo wakulima na wafugaji.

Mafunzo hayo yaliyohusisha mikoa ya Singida na Dodoma yametolewa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kama sehemu ya kuwapa ujuzi mpya waandishi wa habari na watangazaji, kuondokana na uandishi wa mazoea.

Akizungumza katika semina hiyo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, Dkt. Philbert Luhunga amesema lengo la mafunzo hayo kwa waandishi ni kuwajengea uwezo wa kuandika taarifa hizo za kisayansi kwa lugha rahisi, ili waweze kuelewa na kupata matokeo yaliyokusudiwa.