Na Judith Ferdinand, TimesMjira Online, Mwanza
Imeelezwa kuwa uhalifu wa kimazingira ni hatari kwa ustawi wa taifa na dunia kwa ujumla,hivyo waandishi wa habari nchini wameombwa kuchangamkia fursa ya kufanya habari za uchokonozi katika eneo hilo.
Ambapo wanapaswa kushirikiana kwa pamoja na waandishi wa nchi jirani ili kuweza kufanikisha jambo hilo na kuwa na jamii ilio salama na yenye mazingira yalio na uhifadhi bora.
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari wa kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya na uhalifu Tanzania (OJADACT) wakati akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari takribani 50 kutoka mikoa mbalimbali nchini,ambao wameshiriki mafunzo ya siku moja ya namna ya kuripoti habari za uhalifu wa mazingira yaliyofanyika kwa njia ya mtandao.
Mafunzo hayo yameandaliwa na (OJADACT) kwa kushirikiana na shirika la kimataifa la Environmental Reporting Collective (ERC),ambapo Soko amesema kwa pamoja wanawahamasisha waandishi wa habari wa nchini kushirikiana na kufanya kazi za uandishi wa habari za uchokonozi kwa pamoja na waandishi wa habari kutoka nchi jirani kwenye eneo la uhalifu wa mazingira.
Soko amesema, uhalifu wa kimazingira ni hatari kwa ustawi wa dunia hivyo waandishi watumie mafunzo hayo kupata ubobezi wa kuandika habari za mazingira na kuchangamkia fursa hiyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa ERC Ian Lee awali akifungua mafunzo hayo kwa njia ya mtandao,amesema shirika lao lina fungu la fedha kwa ajili kuwapa waandishi wanaotoka kwenye nchi mbili tofauti walio na dhamira ya kufanya uchunguzi wa uhalibifu wa mazingira unaogusa nchi zote mbili.
” Tunaelewa kuwa kuna changamoto ya fedha za kufanya uchunguzi ndio maana tumetenga fungu maalumu la kuwasaidia waandishi wenye dhamira ya kuandika masuala ya uhalibifu wa mazingira,”amesema Lee.
More Stories
AZAKI yawasilisha mapendekezo yao kwa Serikali katika kuboresha Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050
CP.Wakilyamba :Uvamizi maeneo ya hifadhi ya taifa katavi haukubaliki
Watu wawili wanaodhaniwa majambazi wapigwa risasi na Polisi