Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
VYUO vikuu bora kutoka nchi za India, Cyprus, Uingereza, Malaysia na Uturuki vimeleta wawakilishi wake nchini kwaajili ya kuonyesha shughuli zao kwa watanzania wanaotaka kusoma kwenye nchi hizo.
Vyuo hivyo vitafanya maonyesho kwenye Hoteli ya Serena siku ya Jumamosi hii na Jumapili watafanya maonyesho kama hayo kwenye viwanya vya Mapinduzi Square Zanzibar.
Mkurugenzi wa Global Education Link (GEL), Abdulmalick Mollel, ambaye ndiye mwenyeji wa vyuo hivyo aliyasema hayo jana wakati akizungumzia ujio wa vyuo hivyo.
Aliwataka vijana watanzania kuchangamkia fursa hiyo kwa kuhudhuria maonyesho ya vyuo hivyo ili wachague kozi wanazotaka kwenda kusoma nje ya nchi.
Alisema baadhi ya vyuo vikuu vilivyokuja vinafundisha uhandisi wa meli, urubani na baadhi vina viwanda vya kutengenezea magari.
“Kuna vyuo vimepunguza ada za masomo ya udaktari wa tiba kutoka shilingi milioni 30 kwa mwaka hadi shilingi milioni 10 kwa mwaka hii tunaona ni furs sana kwa watanzania kuchangamkia na watakaofika watapata udahili siku hiyo hiyo bure,” alisema Mollel
Alisema nchini India vyuo ambavyo vimeleta wawakilishi wake ni pamoja na Lovely professional (LPU), ambacho kimebobea kwenye elimu ya uhandisi na biashara, Chuo Kikuu cha MMU ambacho kimebobea kwenye elimu ya tiba na uhandisi na Chuo Kikuu cha Sharda ambacho kimebobea kwenye elimu ya Tiba, Sanaa na Biashara.
Alitaja vyuo vingine kuwa ni vya Cyprus kama Near East University kilichoko Kaskazini mwa nchi hiyo, Chuo Kikuu cha Kyrenia wakati nchi ya Uturuki vyuo vilivyokuja ni Gelism na Ishiki na Malasyia ni Chuo Kikuu cha Segi.
Alisema vyuo vikuu vya Uingereza navyo vitakuwepo kupitia taasisi ya British Council.
Alisema India ina vyuo vikuu vingi hivyo vyuo vikuu ambavyo GEL imeviomba vije ni vyuo vikuu bora nchini humo na kwamba vimeletwa kimkakati.
Alisema vyuo hivyo vinatoa kozi ambazo nyingi hazitolewi kwenye vyuo vya ndani na hata kama zinatolewa ni chache.
“Tumeleta vyuo vikuu vilivyobobea kwenye uhandisi wa aina zote mafuta, gesi madaraja reli kwasababu tunaona ujenzi wa reli ya kisasa SGR kwa hiyo tunatambua uhitaji wa wataalamu wa ina hii hapa Tanzania siku zijazo,” alisema Mollel
Alisema wameleta pia vyuo ambavyo vitawafundisha vijana kusimamia mifumo ya kwenye mafuta na gesi kma bomba la kutoka Hoima Uganda kwenda Tanga.
“Baada ya bomba kujengwa kuna wataalamu wengi sana watahitajika ambao ni watanzania sasa lazima wawe na utaalamu wa kufanyia matengenezo bomba hilo na kulisimamia,” alisema
Alisema Tanzania inaendelea kukua kiuchumi na kiteknolojia hivyo inahitaji wataalamu wengi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).
“Tumeita vyuo ambavyo vinatumia teknolojia ya hali ya juu sana hivyo mwanafunzi wa kitanzania akisomea vyuo hivyo vilivyobobea kwenye TEHEMA anakuwa na msada mkubwa kwa nchi yetu,” alisema
Alisema miongoni mwa vyuo hivyo vimebobea kwenye tiba na vifaa tiba na kwamba uwekezaji mkubwa uliofanywa na serikali katika sekta ya afya umeongeza uhitaji wa wataalamu kwenye sekta hiyo.
“Tunaposema wataalamu wa sekta ya afya hatuzungumzii madaktari tu kuna kozi mtambuka ambazo kwenye sekta ya afya hazifundishwi ama zinafundishwa lakini nafasi ni chache sana mfamo wanateknolojia wa tiba ya moyo wanahitajika sana kwasababu matatizo ya moyo yanaongezeka,” alisema
Alisema serikali imekuwa ikifanya juhudi kubwa kufanyia matengenezo vyumba vya upasuaji kwenye hospitali zote nchini hivyo kuna uhitaji wa kuwa na watalaamu wengi wa kufanya kazi kwenye vyumba hivyo .
“Kwenye vyumba vya upasuaji kunahitajika wataalamu wa usingizi wengi kwasababu huwezi kufanya upasuaji bila kuwa na daktari wa usingizi kwa hiyo lazima tuwe na watalaamu wengi sana na vyuo hivi vinatoa kozi zote hizo,” alisema
Alisema wanahitajika pia wataalamu wa kuwangalia wagonjwa wanapotoka kwenye vyumba vya upasuaji na kwenda kwenye vyumba vya uangalizi maalum (ICU).
Wakati huo huo, Mollel aliwataka watanzania kuchangamkia Shahada za Uzamivu (PhD), zinazotolewa na vyuo vya nje kwa bei rahisi ili kuongeza idadi ya wataalamu na wahadhiri wa vyuo vikuu nchini.
Alikuwa akizungumzia maonyesho ya vyuo vikuu vya Cyprus, Uingereza, Uturuki, Malasyia na India yanayoanza leo Jumamosi kwenye hoteli ya Serena Dar es Salaam.
Alisema kuna baadhi ya watu wanaogopa kusoma Shahada za Uzamivu wakidhani kwamba zinagharama kubwa wakati nje ya nchi mafunzo hayo hutolewa kwa bei rahisi.
“Nitoe wito kwa wanafunzi wanaohitaji kusoma PhD mara nyingi wanafikiri vyuo vikuu nje ya nchi ni ghali sana na tunapokuwa na watu wengi wenye elimu ya kiwango hicho watatusaidia sana kujenga nchi yetu kwenye elimu,” alisema
“Sasa kwa mfano hivi vyuo ambavyo nimeleta mfano vyuo vikuu vya India, Cyprus, Uturuki PhD ni Dola 1,000 za Marekani hapo naongelea shilingi milioni mbili mpaka milioni nne kwa mwaka kwa kiwango cha PhD ni nafuu sana kwasababu kuna vyo hapa ndani gharama zinaweza kufikia hadi Sh milioni nane,” alisema Mollel
Alisema kama mwanafunzi anaweza kupata fursa ya kusoma Shahada ya Uzamivu kwa shilingi 2,300,000 mpaka 4,000,000 gharama hiyo kwenye vyuo vikuu mashuhuri duniani ni fursa kubwa.
“Kwa kuwa vyuo hivyo sasa viko nchini naona ni fursa ya sisi kuongeza idadi ya wahadhiri wanaotamani kusoma ngazi ya Uzamivu tusiogope gharama hizi za vyuo vya nje gharama zake ni ndogo na nafasi zipo,” alisema Mollel
Alisema leo Jumamosi na Jumapili vyuo hivyo vitakuwa na maonyesho makubwa ya elimu kuwapa fursa wanafunzi watanzania wenye mahitaji ya masomo kwenye nchi za nje.
Alisema maonyesho hayo yatafanyika katika ukumbi wa Serena kuanzia asubuhi hadi jioni na kwamba Jumapili yatafanyika kwenye viwanja vya Mapinduzi Square Zanzibar na baada ya maonyesho hayo vitaendelea na udahili wa wanafunzi.
Alisema kuanzia siku ya Jumatatu tarehe 27 vitakuwa vinadahili wanafunzi wanaotaka kusoma nje ya nchi katika ofisi za GEL jijini Dar es Salaam hadi mwezi ujao. “Kuna vyuo vimepunguza ada za masomo ya udaktari wa tiba kutoka shilingi milioni 30 kwa mwaka hadi shilingi milioni 10 kwa mwaka hii tunaona ni furs sana kwa watanzania kuchangamkia na watakaofika watapata udahili siku hiyo hiyo bure,” alisema Mollel
Alisema nchini India vyuo ambavyo vimeleta wawakilishi wake ni pamoja na Lovely professional (LPU), ambacho kimebobea kwenye elimu ya uhandisi na biashara, Chuo Kikuu cha MMU ambacho kimebobea kwenye elimu ya tiba na uhandisi na Chuo Kikuu cha Sharda ambacho kimebobea kwenye elimu ya Tiba, Sanaa na Biashara.
Alitaja vyuo vingine kuwa ni vya Cyprus kama Near East University kilichoko Kaskazini mwa nchi hiyo, Chuo Kikuu cha Kyrenia wakati nchi ya Uturuki vyuo vilivyokuja ni Gelism na Ishiki na Malasyia ni Chuo Kikuu cha Segi.
More Stories
AZAKI yawasilisha mapendekezo yao kwa Serikali katika kuboresha Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050
CP.Wakilyamba :Uvamizi maeneo ya hifadhi ya taifa katavi haukubaliki
Watu wawili wanaodhaniwa majambazi wapigwa risasi na Polisi