Na Jackline Martin, TimesMajira Online
Vyombo vya usalama vimeombwa kushughulika na watu wote wanaotaka kuvuruga amani ya nchi ili watanzania waweze kuendelea na shughuli zao kwa usalama
Hayo ameyasema Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama wakati akizungumza na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam
“Wapo baadhi ya watanzania ambao hawana nia njema na nchi yetu ambao huwa wanapenda kuivuruga amani ya nchi yetu, ninaomba viongozi washughukile na suala hili.”
“Kila Mtanzania anahaki ya kufanya shughuli zake kwa amani na utulivu na kwenda eneo Moja ama jingine kwenda kufanya shughuli zake”
Aidha Msama ameishukuru kamati kuu ya Chama Cha Mapinduzi lakini pia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi nzuri anayoifanya kwaajili ya Kuhamasisha wawekezaji kuja nchini Tanzania.
“Rais wetu amezidi kuita wawekezaji kuhakikisha kwamba wawekezaji wanakuja kuwekeza katika nchi yetu ili kuweza kuinua uchumi wa nchi”
Pia Msama ameishukuru serikali kwa kutoa elimu kuhusu uwekezaji huku akiwataka wale wanaoendelea kupotosha watanzania kuhusu uwekezaji unaofanyika nchini kuacha mara moja
“Naishukuru kamati kuu ya CCM kwaajili ya kuendelea kuelimisha watanzania juu ya uwekezaji katika nchi ya Tanzania.Watanzania wengi sasahivi wameanza kuelewa kuhusu uwekezaji kwasababu wengi walikua wanapotosha kuhusu uwekezaji katika nchi yetu ya Tanzania” Amesema Msama
Kadhalika Msama amewataka wale wote wanaomkashfu Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan mitandaoni kuacha mara moja kwani Rais huyo anaendelea kufanya kazi kubwa nchini ya kulitumikia Taifa
More Stories
Kiswaga:Magu imepokea bilioni 143, utekelezaji miradi
Zaidi ya milioni 600 kupeleka umeme Kisiwa cha Ijinga
Kamishna Hifadhi ya Ngorongoro atakiwa kupanua wigo wa Utalii nchini