Na Aveline Kitomary , TimesMajira Online, Dar es Salaam
MZIO au Aleji kama inavyojulikana na wengi ni hali ya mwili kupata athari (rection) kwa kitu cha kawaida na inachukuliwa kama wadudu wanaoweza kuleta madhara.
Aleji ya chakula inatokana na mapokeo ya mwili kutokana na virutubisho vya protini ambavyo vipo katika vyakula tunavyokula kila siku.
Virutubishi hivi vinaweza kukisiwa kama vitu vyenye madhara kilichoingia mwilini lakini ni vyakula vya kawaida tu.
Mtu anapokula chakula kinameng’enywa na kuingia kwenye mfumo wa mwili huku mwili huo ukitengeneza kinga kwenda kinyume na vile virutubishi vinavyotengenezwa kinga hii kwa kitaalamu tunaiita Emoglobin IG.
Unapokula chakula kwa mara kwanza unaweza usipate athari( reaction) lakini ukija kula tena chakula kwa mara ya pili ukapata madhara.
Aleji huweza kumpata mtu yoyote pale ambapo chakula kitamkataa.
Katika jamii aleji imekuwa sio kitu cha kuzingatiwa sana kutokana na kuamini kuwa hakuna matibabu zaidi ya kuacha kile mbacho kinamdhuru mtu baada ya kula.
Hali hivyo husababisha mahudurio kuwa hafifu katika vituo vya afya hivyo ugonjwa huo kutokutiliwa umakini.
Ni asilimia 15 hadi 25 tu ndio wanaokutwa na tatizo la aleji huku kati ya watoto watano, mmoja anatatizo hilo.
Tatizo hili la aleji linaweza kurithiwa kutoka kwa kizazi kimoja kwenda kwa kingine huku katika nchi za Afrika tatizo ni dogo zaidi ikilinganishwa na bara la Ulaya.
Hata hivyo kasi ya kwenda kutafuta matibabu huenda ikawa chanzo cha kuonesha tatizo kuwa dogo.
Huku pia utofauti wa kinga mwili kuwa imara ukitajwa kwa bara la Afrika kulingana na mazingira.
ASIMULIA ALIVYOPUUZI ALEJI
Ashura Maulid anasema yeye aliweza kuugua aleji kwa kipindi cha miaka nane huku katika siku hizo zote asijue nini kilichokuwa kinamsibu.
Awali alikuwa hautilii maanani ugonjwa huo ila baada ya kuona kuwa hali yake haitengamai akaamua kwenda hospitali
“Siku niliyoenda hospitali nilikuwa na shauku kubwa ya kutaka kujua nini kinanisibu baada ya vipimo wakaniambia nina aleji ambayo inaniletea shida.
“Baada ya kwenda katika hospitali hiyo wakaniambia kuwa kuna vyakula ambavyo sitaki kuvitumia,”anasema Ashura.
Anabainisha kuwa vyakula vinavyomsababishia aleji ni vyama ya kuku na maziwa.
“Lakini kuna vitu vingine ambavyo pia sitakiwi kuvipata au kugusa kama sehemu yenye vumbi na manyoya ya nguruwe pia nina aleji nayo,”anaeleza.
Kutokana na hali yake ya kuchagua vyakula Ashura anasema kwasasa yuko makini zaidi hasa pale anaponunua vyakula.
“Japo Sijakatazwa kutumia vitu vingi ili kuku ndio alikuwa ananisumbua sina la kufanya kwasababu ninapenda sna akula nyama hizo .
“Hata hivyo masharti niliyopewa yamebadilisha mfumo wa maisha yangu sasa Mara nyingi nakula nyumbani huwa sipendi migahawani kutokana na wasiwasi wa uhakika wa chakula kinachoandaliwa.
Ashura anasema kutokana na athari ya aleji hajawahi kupoteza fahamu ila alikuwa anajikuna hadi kufikia hatua ya kutokwa na damu
Hata hivyo anatoa wito kwa watu wasiopenda kuwa na kawaida ya kupima afya zao waende hospitali badala ya kutumia dawa kiholela .
“Nawaambia watu wasiwe kama mimi nilichukua muda mrefu kwenda hospitali kutokana na kupuuzi hadi pale nilipoona nazidiwa ni muhimu kwenda hospitali hasa pale unaopoona kuna hali isiyo ya kawaida katika mwili.
MADHARA YA ALEJI
Aleji hupuuziwa katika jamii baada ya kuwa na madhara madogo na ya muda mfupi katika mwili.
Daktari Mbobezi wa masuala ya Aleji Kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) Dk Kassim Babu anasema kuwa kuna madhara makubwa yanayoweza kusababishwa na aleji katika mwili.
Anasema bado hakuna mkazo wa ugonjwa wa aleji hivyo kwa mara ya kwanza ameamua kuanzisha Jumuiya ya madaktari bingwa wa aleji (ASAT).
Dk Babuu ambaye pia ni mkufunzi katika chuo Kikuu Kishiriki cha Muhimbili (MUHAS) anasema haya”Kwa ufupi kabisa ASAT ni jumuiya mpya kwasababu idara ya aleji ni changa nchini na nimeona ni busara kuanzisha chama ili kiweze kusaidia madakatari wengine kuweza kusoma na hawa waliopo hapa waongeze ujuzi.
“Mimi ni mwenyekiti wa jumuiya hiyo tuko 15 tunatoa hamasa kwa wengine kujiunga na ndani ya mwaka huu tutakuwa na warsha na semina mbalimbali ,”anasisitiza.
Anasema kuwa madhara ya aleji yanagawanyika kulingana na mfumo wa mwili huku mwanzoni dalili zikiwa ni mdomo kuwasha,kuvimba mdomo ,kuvimba koo,mwili kuwashwa na mtu anapojikuna anavimba.
“Katika mfumo wa upumuaji unaweza kuwa kikohozi ,kifua kubana ,ukipumua unatoa aina ya sauti kama filimbi.
“Kwenye mmeng’enyo wa chakula inaweza kutokea kuharisha,kutapika hata tumbo kuuma na zingine,”anaeleza.
VYAKULA VINAVYOWEZA KULETA ALEJI
Dk Babu anasema vyakula vinayoleta kuleta aleji kwa baadhi ya watu ni aina zote za karanga kama nuts,karanga za kulima na zingine ,kingine ni maziwa ,samaki, soya na ngano.
“Tunashauri kwamba kwa vile vyakula ambavyo vinaleta aleji aviache kwa wiki nne mpaka sita baada ya hapo tunafuatilia moja moja na kama ni ngano au kingine ikileta rection tunamwambia aache.
“Na pia tunaelekeza njia mbada mfano kama ni maziwa ya ngo’mbe anaweza kutumia mengine atajaribu ya mbuzi,ngamia na mengine na kama ni samaki tunaangali ni wa aina gani na maji gani halafu tunamwambia ajaribu wa maji ya baridi badala ya moto.
“Kwa Samaki wale wenye magamba tafiti nyingi zinaonesha kuwa ni watu wachache wanakuwa nayo na kwa karanga tunamyima asiendelee kutumia labda kwa kipindi matibabu yatayopatikana,”anaeleza Dk Babu
Anasema ni changamoto zaidi kuacha kutumia maziwa kutokana na kutumika katika kutengeneza vitu vingi kama choclet,biskuti na mengine.
APINGA TIBA MBADALA
Dk Babu anatoa wito kwa watanzania wote wenye magonjwa ya aleji kama mafua ya mara kwa mara, kuwashwa ngozi,pumu,kubanwa kifua ,aleji ya chakula wawaone madaktari na kupata ushauri.
“Njia za tiba mbadala kwa aleji nasema sio nzuri kuna dawa zinazosaidia kutuliza dalili na kuondokana kabisa na shida anayopata,”Alnasisitiza.
KINACHOPASWA KUFANYIKA
Dk Babu anasema kuna vitu mbalimbali ambavyo vinatakiwa kufanya katika kuidhibiti aleji ambavyo ni
“Kuangali rection inayotokea hapa tunagawa katika sehemu tatu ambayo ni mail reaction,civial rection na moderate reaction.
“Kwa zile mail na moderate ukipata dawa huwa inatulia lakini kwa civial unaweza kupata athari kubwa ya chakula wakati mwingine kupoteza hata fahamu ,presha ikashuka,mapigo ya moyo kuongezeka inabidi mgonjwa awahishwe hospitali ili kuchomwa sindao.
Anasema kuwa endapo mtu akila chakula kikaleta madhara kwa mara ya kwanza ni bora aache mara moja ktumia aina hiyo.
“Hatua ya pili ni kujaribu kutafuta dawa za kutibu dalili za aleji kwa kawaida aleji haitibiki ila zile dalili ndo zinazuiwa hadi baadae dawa utakapogunduliwa ambayo itasaidia lakini kwa nchi zilizoendelea zipo ila kwetu bado haijafika.
“Tuna dawa kama immunity therapy ,small dose ya kile kitu cha mtu kuwa na aleji ,”anabainisha.
UTENGENEZAJI WA BIDHAA KUEPUKA ALEJI
Kwa upande wake mmoja wa wajasirimali,Jamila Manengelo anasema kuwa yeye anapotengeneza bidhaa zake anazinatia zaidi kuwepo vitu vinavyotajwa kuwa na aleji mara kwa mara.
“Tunatengeneza product za unga na unga wetu unaitwa sweet unga ambao unanafaka ndani na hizo nafaka zinashauriwa na Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) kwa watoto kuanzia miezi sita na kuendelea.
“Uchanganyaji wa karanga na unga wakati mwingine unaleta aleji kwa mtoto Lakini katika product yangu siweki karanga na wengi wananishangaa lakini kinamama hawajui kuwa kunauwezo wa madhara katika kutumia karanga.
“Nimekutana na watu ambao wana aleji na soya,karanga kipindi nimetengeneza unga na soyo nilipata kesi za aleji kwa watoto hiyo nikawa nachakua nafaka za kuchanganya katika unga wangu,”anaeleza.
Anasema wazazi wengi hawana uelewa wa namna ya kundaa lishe za watoto ambazo haziwezi kusababisha aleji.
“Ni muhimu wakaelewa hili wengine wanaanda tu ili mradi na hata ikitokea mtoto anaaleji wengine hawafatilii.,”anashauri Jamila.
KUNA HAJA YA JAMII KUELEWA
Mtaalamu wa lishe kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe (TFCN) Glanasema uelewa wa jamii kuhusu aina za nafaka ambazo zinaweza kusababisha aleji ni muhimu ili kuepuka madhara kwa urahisi.
Anasema mwitikio wa mwili baada ya kupata aina ya chakula Fulani huweza kuwa tofauti kama matariajio ya mlaji.
“Mwitikio wa mwili baada ya kupata aina fulani ya chakula kwamba katika kile chakula kunachembe chembe ambazo zinagusa kinga mwili hivyo kufanya kureact na baada ya hapo inaanza kupamba na kile ambacho mwili inaweza kukupa ndo unakuja kupata zile dalili mbalimbali.
“Mwili unatengeneza kemikali ambazo hunaanza kupambana na protini iliyoingia ambayo inatokana na samaki na mwili utaanza kuwasha kutoka na mpambano kati ya hivyo vitu unajikuta unawashwa, umevimba zinatofautiana kwa kila mtu.
“Ni kinga mwili inaamua kupambana na kitu kigeni kwa kukiona ni kibaya hivyomfano mwingine anakunywa maziwa anaharisha na mwingi haaharishi huu ni upinzania ndani ya mwili na mapokeo yanatofautina na sio chakula tu hata mazingira yanachangiana hali hivyo inapotokea ni vyema kujua chanzo ni nini na kuacha kula aina hiyo ya chakula hata katika bidhaa za nyama samaki aleji inategemea na aina ya samaki,”anasema.
UNYONYESHAJI HUKINGA
Mtaalamu huyo anasema endapo mtoto anatanyonyshwa ipasavyo uwezekana wa kutokupa aleji ni mkubwa tofauti na ambaye hajanyonyeshwa ipasavyo.
“Kwa watoto ambao hawajanyonyo maziwa ya mama ipasavyo wanakuwa wanapata aleji mtoto anapozaliwa anatakiwa kupewa maziwa ya mama pekee kwa kipindi cha miezi sita hii itsaidia.
KUHUSU MATUMIZI YA UNGA WA LISHE
Anasema watu wengi wanatengeneza unga nyumbani au kununua na kuuita unga wa lishe huku kukiwa hakuna uhakika wa kiwango cha unga huo.
Anabainisha kuwa watu wasijididangaye na kuacha kuwapa watoto wao vyakula kwa kuamini unga huo pekee.
“Unga wa lishe ni nafaka imechangaywa na jamii ya mikunde kama soyo ,dagaa,karanga na sisi kama wataalamu hatutaki kuuita unga wa lishe sisi tunaita unga mchangayiko wa nafaka hii imefanya jamii iamini unga huo na kuona hakuja haja wa watoto kupewa unga huo tu bila vitu vingine.
“Kuna kiwango na virutubishi vya protini na kabohyreti kinachokubalika kama haijafikiwa tunawezea kusema sio unga sahihi .
“Kiwango cha protini kinatakiwa kisiwe chini ya 70 kuna viasili nane sasa mchangayiko huo tunaweza kupata protini na pia zipo maabara zinazopima unga wa lishe kwa viwango vinavyokubalika hivyo ni vyema watu wakaangalia nembo ya TBS ili kujua kama kunaubora,”anasisitiza
More Stories
Ubunifu wa Rais Samia kupitia Royal Tour unavyozindi kunufaisha Tanzania
Rais Samia anavyojenga taasisi imara za haki jinai kukabilina na rushwa nchini
Rais Dk. Samia alivyowezesha Tanzania kuwa kinara usambazaji umeme Afrika