December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Vodacom yatoa sh.500,000 washibdi droo ya ‘Ni Balaa’

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online. Dodoma

KAMPUNI ya Tknolojia na Mawasiliano, Vodacom Tanzania (PLC), Agosti 4, 2024 iliwazawadia washindi wawili kiasi cha Sh 500,000 kila mmoja baada ya kushinda kwenye droo ya kwanza ya kampeni mpya ya “Ni Balaaa” Kila Mtu ni Mshindi” katika maonesho ya Nane Nane yanayoendelea jijini Dodoma.

Kampeni hiyo ambayo itaendeshwa kwa muda wa miezi mitatu ikiwa imeamza Agosti 4, mwaka huu na kutarajiwa kumalizika Octoba, Ina lengo la kunufaisha wateja na jamii kwa ujumla na kuhakikisha kila mshiriki anapata nafasi ya kushinda zawadi zikiwemo za kila siku, wiki na mwezi, pamoja na washindi watano wa zawadi kuu.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mkuu wa Kanda ya Kati wa Vodacom Tanzania, Joseph Sayi, amesema, “Mwitikio kutoka kwa wateja wetu umekuwa mzuri sana hivyo tunafurahi kuona washindi wengi tayari wepatikana na kila muamala wa M-Pesa wakati wa kampeni unaongeza nafasi yako ya kushinda, iwe unatuma pesa kwa familia, unalipia bili au unatumia M-Pesa super app, kila muamala unahesabika.”

Kampeni hiyo yenye kaulimbiu ya “Kila Mtu ni Mshindi!”, itaendelea hadi Oktoba, ambapo kwa upande wa Washindi wa kila siku watapata Sh.100,000, washindi wa kila wiki Sh.500,000, washindi wa kila mwezi Sh. Mil 1 na washindi watano wa zawadi kuu kila mmoja atapata Sh. Mil 20 na kufanya jumla kuu kuwa Sh. Mil 100.

Pia, washindi hawa watano watapata fursa ya kipekee ya kuchagua shule ambayo Vodacom itasaidia shule hiyo kuboresha mazingira ya kusoma na haswa maktaba.

Aidha, Emmanuel Chima, aliyetangazwa kuwa mmoja wa washindi wa kila siku, akiwa mwenye furaha alisema, “Nilishangaa na nafurahi sana kushinda Sh.100,000! Ni ajabu kwamba kutumia tu M-Pesa unaweza kuwa mshindi wa zawadi nzuri kama hizi. Ninawahimiza kila mtu kushiriki.”

Sayi amesema, kampeni ya “Ni Balaaa” imeundwa kuwa shirikishi, ikiruhusu kila mtu kushiriki, bila kujali wapi walipo au hali zao za kiuchumi kwani M-Pesa inarahisisha kila mtu kushiriki, ikiwemo wamiliki wa biashara ndogo ndogo kutoka popote nchini.