Na Mwandishi Wetu,Timesmajiraonline,Zanzibar
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Alhaj Othman Masoud Othman, leo Ijumaa Oktoba 6, 2023 amejumuika na Viongozi wa Kitaifa pamoja na Waumini wa Kiislamu katika Ibada ya Sala ya Ijumaa, huko Mkwajuni Kidombo, Wilaya ya Kaskazini A, Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Baada ya Ibada hiyo, iliyohudhuriwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dokta Hussein Ali Mwinyi, Mheshimiwa Othman ameshiriki pia katika Khitma na Dua Maalum ya kuwaombea Viongozi, Masheikh na Wazee waliopo hai na ambao wameshafariki dunia, ndani na nje ya Kijiji hicho.
Harakati zote hizo ni sehemu ya Mwitikio wa Viongozi, kufuatia Mwaliko wa Kila Mwaka wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tano ya Zanzibar, Alhaj Dokta Salmin Amour Juma, unaoambatana na Sherehe za Maulid ya Mtume Muhammad (SAW), kiijijini hapo.
Viongozi mbali mbali wa Serikali, Dini, Siasa na Jamii, wakiwemo Rais Mstaafu wa Zanzibar wa Awamu ya Saba, Alhaj Dokta Ali Mohamed Shein; na Mufti Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Saleh Omar Kaabi, wamehudhuria katika Hafla hiyo.
Kabla ya Swala hiyo, Khatib wa Khutba Mbili katika Ibada hiyo, Sheikh Abdulkarim Said Abdulla kutoka Ofisi ya Mufti wa Zanzibar, ameukumbusha Umma wa Kiislamu juu ya Mapenzi kwa Mtume Muhammad (SAW); kuwapenda Viongozi,sambamba na Wenye Mamlaka kuwapenda na kuwahurumia raia.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba