November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Viongozi wa vijiji waonywa kujigeuza kuwa Mahakama

Na Israel Mwaisaka, TimesMajira Online, Nkasi

MWENYEKITI wa halmashauri ya wilaya Nkasi Pankrasi Maliyatabu amewataka viongozi wa vijijji na kata kuacha kuutumia muda mwingi kukaa ofisini na kusikiliza kesi na kuacha jukumu lao la msingi la kuhamasisha na kusimamia maendeleo na jukumu hilo la kesi wangeziachia Polisi na Mahakama.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika vijijji vya Mkole na Ipanda kata ya Nkomolo amedai kuwa shughuli nyingi za maendeleo zimekuwa zikisuasua na kumbe viongozi wa vijiji na kata wamejigeuza na kuwa ni Polisi na Mahakama wakati mamlaka hizo zipo na kupelekea shughuli za maendeleo kukwama katika maeneo yao.

Hilo limekuja baada ya mkazi mmoja wa kijiji cha Ipanda Michael Mhoja kumweleza mwenyekiti wa halmashauri kuwa kukwama kwa ujenzi wa zahanati kijijini hapo kumetokana na viongozi wao wa kijiji kuutumia muda mwingi kusikiliza kesi ofisini na kushindwa kabisa kusimamia shughuli za maendeleo.

Kufuatia hari hiyo mwenyeki wa halmashauri aliutumia mwanya huo kuwapiga marufuku viongozi wa vijiji kuacha kazi ya kusikiliza kesi badala yake wawaongoze Wananchi wao na kesi zao Polisi ambao watakua na jukumu la kuwapeleka Mahakamani na si kujigeuza wao na kuwa mahakama na kuwa kufanya hivyo ni kwenda kinyume na sheria.

“Haiwezekani kabisa viongozi wetu wa vijiji mkaacha jukumu lenu la msingi la kusimamia maendeleo mnakimbilia kufanya kazi za mahakama na kusahau jukumu lenu la msingi la kusimamia maendeleo kupeleke kazi zenu kudoda kiasi cha kuanza kufikiria huko kwenye kesi mnakokimbilia kuna nini? Alisema Pankrasi

Pia amewataka viongozi hao wa vijiji kuhakikisha kwamba Wananchi wao wanafanya kazi za kujiletea maendeleo kwa kuwachukulia hatua wale wote wanaokunywa pombe asubuhi badala ya kwenda kufanya kazi.

Amesema kuwa wengi ya watu wamekua masikini kwa kuendekeza ulevi wakati kazi za kufanya zipo,hivyo sasa kila mmoja ashiriki katika ujenzi wa taifa kwa kufanya kazi na wasisite kuwachukulia hatua watu wa namna hiyo kwani wanarudisha nyuma jitihada za taifa za kujikwamua kiuchumi.

Hivyo amewapa muda wa wiki tatu wenyeviti wa vijiji na vitongoji kuhakikisha miradi yao ya shule na afya iliyokwama inakamilika baada ya hapo wale watakaoshindwa kufikia lengo watachukulia hatua za kinidhamu.

Mwenyekiti huyo wa halmashauri yupo ziarani kukagua shughuri za maendeleo ikiwa ni pamoja na kusikiliza kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi wa haraka kero hizo.

Mwenyekiti wa halmashauri wa tatu kutoka kushoto Pankrasi Maliyatabu akiangalia choo cha shule ya msingi Kanazi kilichotelekezwa huku Wanafunzi wakikosa choo salama
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wakitoa kuero zao mbele ya mwenyekiti wa halmashari