November 7, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Viongozi wa kiimani Mkoani Tanga waitaka serikali kuongeza msisitizo mapambano dhidi ya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia nchini

Na Hadija Bagasha, TimesMajira Online, Tanga

Viongozi wa kiimani Mkoani Tanga wameitaka serikali kuongeza msisitizo kwenye mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia ambavyo vimekuwa vikiripotiwa maeneo mbalimbali nchini.

Mchungaji wa kanisa la waadventista wasabato JIjini Tanga Julias Mbwambo ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.

Mchungaji Mbwambo ametoa kauli hiyo muda mfupi mara baada ya kuripotiwa kwa matukio mbalimbali katika jamii yasiyompemdeza Mungu.

“Ni kweli tunaishi katika ulimwengu ambao tabia za wanadamu maadili yameshuka kuna habari nyingi tunazisikia katika vyombo vya habari ikiwemo watoto kulawitiwa jambo hili tunalikemea vikali, “amesema MChungaji huyo.

Awali akizungumzia shule inayosimamiwa na kanisa hilo Mchungaji Mwambo amesema wana mipango mbalimbali ya kuhakikisha wanafika mbali zaidi ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanafunzi waliopo shuleni hapo wanapata elimu bora kulingana na mitaala ya serikali iliyopo.

“Tunatamani kama wanatanga ifahamike na siku moja tutoke kwenye zile kumi bora bali tuwe wa kwanza kitaifa Miradi mbalimbali inaendelea ikiwemo ujenzi wa madarasa project hii ya, madarasa inayoendelea yatakapokamilika yatawafanya wanafunzi tulio nao waweze kusoma vizuri, “amesisitiza Mchungaji Mbwambo.

Akizungumzia suala la ujenzi wa shule ya sekondari ya kanisa hilo katika eneo la Ngomeni wilayani Muheza mchungaji huyo amesema kuwa wanaendelea na mchakato wa kukamilisha vibali ili ujenzi uanze mara moja.

“Jambo hili tumelifanya baada ya kupokea maoni na mawazo kutoka kwa wazazi ambao wanasomesha watoto wao katika shule yetu ya msingi kutokana na namna tunavyowalea kimaadili na kiroho, “alisisitiza Mbwambo.

Kwa upande wake Mwalimu mkuu wa shule ya Kana Central Andrea Lazaro amesema kuwa mikakati yao ni kuwahimiza walimu kufundisha vizuri ikiwa ni pamoja na kuwapatia motisha pindi wanapofanya vizuri.

Mwalimu Mkuu huyo amesema kuwa wanatarajia kuongeza kiwango cha ufaulu shuleni hapo ili kuletea sifa ya Mkoa wa Tanga jambo ambalo amesema linapaswa kuungwa mkono.

“Licha ya shule yetu kuwa chini ya kanisa la waadventista wasabato lakini shule hii haina ubaguzi wa aina yeyote ile hapa tuna madhehebu yote ya kikristo na dini zote ambapo katika mwezi mtukufu huu wa ramadhani wakati wa mchana wanafunzi wanapelekwa msikitini kwa gharama ya shule kwenda na kurudi hii inaonyesha ni namna gani tunajali imani za watu wengine, “Amesema Lazaro.

Mwalimu wa taaluma shuleni hapo Samweli Bendera amesema taaluma shuleni hapo ni nzuri kwani wamejikita katika ufundishaji na kuhakikisha ujifumzaji wa waoto unakuwa wa kiwango cha juu ambapo mpaka sasa wamekuwa na wanafumzi wanaofanya vizuri zaidi katika nafasi za kimkoa na kitaifa kwa ujumla.

Baadhi ya wanafunzi shuleni hapo akiwemo Tresure Asifiwe na Suleiman Baraka wamemshukuru Rais Samia kwa kuwaboreshea sekta ya elimu ikiwemo ujenzi wa madarasa ambao ameufanya hivi karibuni.