January 11, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Viongozi wa dini wakunwa na Rais Samia kumtengua Gekul

Na Mwandishi Wetu,TimesmajiraOnline,Dar

VIONGOZI wa dini nchini wametangaza kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan, kwa hatua alizozichukua kutengua uteuzi wa aliyekuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Sheria na Katiba, Pauline Gekul, kwani amedhihirisha hakuna aliye juu ya sheria.

“Hata kama sababu za Rais Samia kutengua uteuzi wa Gekul hazikuelezwa, lakini ili kukomesha kiburi cha wanasiasa wanaolewa madaraka, wanaotia aibu Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na mwanamke mahili kwa upendo, kwa tunayoyaona mtandaoni sisi viongozi wa dini yakimhusisha mwanasiasa huyo, tunampongeza Rais Samia kwa uamuzi huo.”

Kauli hiyo imetolewa kwa niaba ya viongozi wa dini na Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Maaskofu na Makhehe ya Maadili, Amani na Haki za Binadamu kwa Jamii ya Madhehebu ya Dini nchini, Askofu William, Mwamalanga kupitia taarifa yake kwa vyomo vya habari aliyoitoa jana.

Kabla ya Rais Samia kufikia uamuzi wa kutengua uteuzi wa Gekul, ilisambaa video kwenye mitandao ya kijamii ikimuonesha kijana mmoja kwenye video akiomba msaada wa kisheria ili aweze kupeleka suala lake kwenye vyombo vya haki akimlalamikia Gekul kwa kufanyika vitendo kwa ukatili.”

Askofu Mwamalanga, amesema madai ya kijana huyo kumtaja, Gekul kwenye yale anayodai kutendewa ukatili uliopindukia na hatari Duniani.

Askofu Mwamalanga ameelezea kushangazwa kuona kiongozi mmoja wa dini akimtetea Gekul na kwamba hicho ni kielelezo cha baadhi ya viongozi kuanza kupoteza mwelekeo.

Alimtaja Rais Samia kama mbunifu kutokana na uwezo wake wa kuinua Taifa.

“Lengo lake ni kuondoa uvivu ndani ya jamii, bahati mbaya hapati watendaji wengi wanaomuelewa. Akipata wanaomuelewa wengi ndani ya Mawaziri na Makatibu wakuu Taifa hili litakuwa mbali,”alisema.

Mbunge wa Babati Mjini, Pauline Gekul

Askofu Mwamalanga amemtaja Rais Samia kama Mama wa ipendo kwa jamii ya Watanzania tofauti na wanasiasa wengine ambao wanapenda kula wenyewe.

Ndani ya mitandano ya kijamii kumekuwa na video inayomuonesha kijana aliyetajwa kwa jina la Hashimu Ally, akidai kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji na kundi la vijana kwa maelekezo ya Gekul.

Ally anadai Gekul aliamuru aingiziwe chupa sehemu ya haja kubwa au kwa madai alitumwa kimkakati kwenda Hoteli ya Paleii Lake View Garden inayodaiwa kumilikiwa na Gekul.

Kupitia mtandao mmoja wa kijamii, wakili wa kujitegemea Peter Madeleka aliandika;

“Kitendo cha kishetani alichofanyiwa Hashimu Ally, kuingiziwa chupa sehemu ya haja kubwa, siyo siasa. Tunataka wote wanaotajwa kuhusika na ushetani huu, wawajibishwe bila kujali vyeo vyao.

Aliyewahi kuwa Meya wa Ubungo, Boniface Jacob kupitia ukurasa wake wa kijamii alishauri haki itendeke.

Kwa upande wake mwanaharakati Maria Sarungi, alitaka kufanyike uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo.