December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Vikundi 200 vya wanufaika wa TASAF kuanzishwa Wilayani Kalambo

Na Israel Mwaisaka, TimesMajira Online, Kalambo

Wanufaka wa mradi wa TASAF wilayani Kalambo mkoani Rukwa wametakiwa kujiunga kwenye vikundi vitakavyo wawezesha kukuza uchumi wa kaya kwa kuanzisha miradi ya pamoja na kupata mikopo itakayo wawezesha kuweka akiba na kujikwamua kiuchumi.

Hayo yamebainishwa na mratibu wa TASAF wilayani humo Mariam Kimashi wakati wa kampeni ya uundwaji wa vikundi kwenye vijiji vya kata za Matai na Lyowa.

amesema kwa kutambua umuhimu wa uwepo wa vikundi, Halmashauri imeanzisha mpango wa kuwaunganisha wanufaika kwenye vikundi na kwamba wanatarajia kuunda vikundi 200 ambapo kila kikundi kitakuwa na wanufaika 15.

‘’lengo la serikali ni kuwaweka pamoja wanakikundi ili kuongeza uchumi wa kaya na kwamba endapo kikundi kitafanya vizuri na kuwa na uwezo basi TASAF itakipatia ruzuku ya uzalishaji ili kuifanya kaya kujikwamua kiuchumi’’alisema Kimashi

Hata hivyo baadhi ya wanufaika wa TASAF wilayani humo wameipongeza serikali kwa kuwawezesha kifedha na kwamba kuanzishwa kwa vikundi hivyo kutaenda kuwaondolea adha ya kuwa tegemezi katika jamii.