November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Vijiji 11 Nachingwea kunufaika na mradi wa Maji safi na salama

Na Mary Margwe, TimesMajira Online, Nachingwea

Jumla ya Vijiji vipatavyo 11 kutoka Kata tatu Naipanga, Chiumbati na Rahaleo Wilayani Nachingwea Mkoani Lindi vinatarajia kunufaika na mradi wa huduma ya maji safi na salama wa Naipanga.

Hayo yalibainishwa jana na Meneja wa Wala wa Maji nanUsafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA ) Wilaya hiyo Mhandisi Sultan Ndoliwa wakati akizungumza na kuutambulisha mradi huo mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mohamed Moyo, wajumbe wa Halmashauri kuu ya Vijiji.

Mhandisi Ndoliwa amesema mradi wa Maji wa Naipanga upo katika kata ya Naipanga ipo katika kata za Naipanga, Chiumbati, Rahaleo na Stesheni

” Mradi huu unajengwa chini ya Mpango wa lipa kwa matokeo ( Payment for Result-PforR ) na kusimamiwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini ( RUWASA )” amesema Mhandisi Ndoliwa.

Aidha amesema Mradi wa Maji wa Naipanga utatekelezwa na Mkandarasi Broadway Engineering Co Ltd- Dar Es Salaam kwa gharama ya sh.bil.1,187,057,785 na VAT kwa muda wa miezi 12 na Utekelezaji wake unaanza rasmi Leo Agost 22, Mwaka huu na kukamilika Agost 22, 2024.

Mhandisi Ndoliwa ameongeza kuwa mradi unatarajia kutoa huduma kwenye Vijiji 11 vya Chiumbati shuleni, Chiwindi, Tandika, Luagala, Rahaleo, Maendeleo, Kilombelo, Naipanga, Nagaga, Joshoni na Chekeleni ambapo utahudumia watu wapatao 19,110 kwa kuzingatia ratiba ya mgawanyo wa Maji ya WANAWASA.

” Mradi una tenki la ujazo wa Lita 300,000 na uzio, vituo vya kuchotea maji vyenye sehemu 2 kila kimoja na Mtandao wa mabombawenye urefu wa kilometa 32,425 ” amesema Mhandisi Ndoliwa.

Aidha alifafanua kuwa kazi zote za mradi zilizopangwa kufanyika zimekamilika ambazo ni Ujenzi wa tenki la maji la ujazo wa Lita 300,000, Ujenzi wa Vioksi 35, Ujenzi wa Vilula ( DPs ) na Uchimbaji mitaro na ulazaji Bomba kilometa 32,425.

Hata hivyo RUWASA inawaomba wanufaika wa mradi huo kuhakikisha inampa ushirikiano Mkubwa Mkandarasi husika ili aweze kufanikisha majukumu yake Kwa wakati uliokusudiwa.