January 8, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Vijana zaidi ya 1000 kupatiwa elimu ya Ufundi wa magari yanayotumia Umeme

Na Queen Lema, TimesMajira Online, Arusha

Chuo cha teknolojia Jema kilichopo Mwanza kwa kushirikisha na Jaica pamoja na Japan wanatarajia kutoa mafunzo Kwa vijana Zaidi ya vijana 1000 ya kutengeneza magari ya umeme lengo halisi ni kuboresha mazingira lakini pia kuibua ajira

Hayo yameelezwa na Elphasi Nguka ambaye ni mratibu miradi kutoka katika Jema Afrika mapema jana wakati akiongea na wageni mbalimbali ambao walitembelea banda la Jema Afrika kwenye maonesho ya NACT VET yanayoendelea Arusha

Alisema kuwa mafunzo hayo tayari yamesharatibiwa na muda mfupi kutoka sasa yataanza kwa kuwa mpaka sasa NACTE wameshaipitisha

“Mpaka sasa NACTE wameshaipitisha na tutaanza kutoa mafunzo ya magari ya umeme na lengo halisi ni kuwafanya vijana wawe na mafunzo na waanze kutengeneza magari kwa kuwa hapa nchini bado kuna uhaba mkubwa wa mafundi WA magari yanayotumia umeme”

Aliongeza kuwa magari ya umeme kwa sasa ndiyo yanaongia Kwa Kasi hapa Tanzania lakini hata Afrika Mashariki lakini kama bado wataalamu hawatakuwepo basi teknolojia hiyo itakuwa ni sawa na bure.

Aliwataka vijana kuhakikisha kuwa wanachangamkia fursa hiyo Kwa kujiunga na mafunzo hayo ili waweza kubobea katika fani hiyo lakini pia kupata ajira

“Sisi kama Jema tunataka kuona kuwa kila mahali ambapo kuna barabara lakini pia hata umeme kuwe na wataalamu wa haya magari ya umeme na pia waweze kutengeneza magari hayo ya umeme ambayo ni rafiki kwa mazingira”aliongeza

Katika hatua nyingine aliiomba Serikali kuweza kufanya wepesi Kwa kutoa vibali hasa kwa wawekezaji sekta ya elimu hapa nchini kwa kuwa kwa sasa wawekezaji wanakwama kutokana na vibali kuchukua muda mrefu sana