Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online, Ngorongoro
UJUMBE wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) zaidi ya Vijana 1,000 wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Taifa Kenani Kihongosi umewasili katika Hifadhi ya Ngorongoro kwa lengo la kufanya utalii wa kutembelea vivutio mbalimbali vilivyopo ndani ya Hifadhi hiyo.
Akizungumza leo Juni 4,2022 , Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Kenani Kihongosi ameeleza lengo la ziara hiyo ni kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwenye filamu ya The Royal Tour ambayo imeonyesha vivutio mbalimbali vilivyopo ndani ya Nchi yetu.
“Vijana hawa zaidi ya 1,000 waliofika Ngorongoro niliwapa wazo hili katika mitandao yetu ya kijamii na kuwaeleza wachangie gharama kufanikisha jambo hili, vijana walikubali na safaribyetubilianzia dodoma hadi Karatu, hapa karatu tumekodisha magari ya utalii 142 na kila gatibwalipanda vijana 9.
Hapa Ngorongoro tumekuja kuona vivutio tulivyonavyo ili kusaidia kutoa hamasa na chachu kwa watanzania wengine wajue kuwa Utalii unaanza na sisi wenyewe ili tuwe mabalozi wa kuhamasisha wageni wengine wa nje ya Nchi kutembelea pamoja na hayo Kihongosi ameweza kuwaonyesha wananchi wa Karatu Filamu ya Royal tour ambayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan alikuwa Muigizaji Mkuu katika Filamu hiyo” alifafanua Kihongosi
Ameongeza uwepo wao katika maeneo ya Wilaya za Karatu na Ngorongoro umesaidia kuongeza mzunguko kwa wajasiriamali hasa Hoteli, Magari ya utalii, biashara za vyakula kwa mama lishe hivyo kusaidia uimarishaji uchumi wa wananchi katika kusukuma agenda ya maendeleo na kuwaambia watu kuwa utalii ni fursa na utalii ni ajira.
Akipokea Ujumbe huo Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Raymond Mangwala amewashukuru UVCCM kwa kuunga mkono jitihada za Rais na Serikali yake kuhamasisha utalii wa ndani kwa vitendo kwa kuamua kuchangishana kwa kwa idadi kubwa kutembelea vivutio vya Ngorongoro kwa pamoja.
Ameeleza kuwa Vivutio vya Ngorongoro ni vya kipekee na baada ya uzinduzi wa Filamu ya Royal tour anaamini wageni wataongezeka na kuongeza mapato ya Serikali ambayo yataongeza uchumi wa Nchi na kusaidia Serikali katika ujenzi na uimarishaji wa huduma zingine za kijamii kwa wananchi wake.
Kwa upande wake Kamishna Msaidizi Mwandamizi Elibariki Bajuta anayesimamia huduma za Ulinzi NCAA ameuhakikishia ujumbe huo kuwa eneo la Hifadhi ya Ngorongoro ni Salama, tulivu lenye vivutio vya Kila aina na Serikali kupitia NCAA inaendelea na juhudi za Uhifadhi na uboreshaji wa miundimbinu ya Utalii ili wageni wanaotembelea Hifadhi hiyo kupata huduma bora muda wote.
More Stories
Rukwa waanzisha utalii wa nyuki
Mhandisi Kundo ataka vyanzo vya maji vitunzwe
Dkt.Kazungu:Megawati 30 za Jotoardhi kuingia kwenye gridi ifikapo 2026/27