December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama, Anderson Nsumba akimwelekeza jambo Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kuhusu Jengo jipya la Utawala.

Vijana kuneemeka mkoani Shinyanga

Na Anthony Ishengoma, Shinyanga

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga, Dkt.Philemon Sengati amezitaka halmashauri za Shinyanga kutengeneza vikundi vya vijana wenye ujuzi na kuwajengea uwezo kwa kuwapa kazi mbalimbali katika miradi inayoendelea katika Halmashauri zao kama kama ambavyo Manispaa ya Kahama ilivyojenga uwezo kwa vikundi hivyo na kuvipa kazi katika jengo jipya la utawala ambalo lipo katika hatua za mwisho kukamilika.

‘’Wakati mkiwa katika hatua za kutayarisha vikundi hivyo na kuvijengea uwezo endeleeni kutoa kazi vikundi hivi vya Manispaa ya Kahama katika miradi yote inayoendelea katika Halmashauri za Shinyanga na hili ni agizo la viongozi wa Mkoa,”ameongeza Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati.

Mkuu huyo wa Mkoa amesema hayo alipofanya ziara Wilaya ya Kahama na kujionea maendeleo ya ujenzi wa Jengo la Utawala la Manispaa ya Kahama na kushuhudia vijana wazawa ambao walisanifu michoro ya jengo na kusimamia ujenzi ikiwemo kupewa kazi ya kuweka thamani katika jingo hilo jipya lenye ubora.

Aidha, Dkt. Sengati ameshauri Manispaa ya Kahama kuendelea kuwajengea uwezo wazawa na kutangaza kazi zao ili waweze kupewa kazi hata katika Nchi jilani ili kuweza kuiletea sifa Tanzania kwani wamefanya kazi nzuri sana kama zile ambazo kwa kawaida zimekuwa zikifanywa na wakandarasi wa kigeni.

Naye Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Batlida Buriani aliwapongeza viongozi wa Manispaa ya Kahama kwa kuwaamini Wahandisi wa kike ambao walisanifu michoro ya jengo na kusimamia ujenzi wa jengo hilo la kisasa tofauti na wengine ambao wangetoa kazi hiyo kwa watu wengine ikiwemo raia wa kigeni.

‘’Katika hali ya kawaida ya mfumo dume isingekuwa raisi kwa nyinyi kuwaamini mabinti awa lakini nyie mumekwenda mbele zaidi na kuwapa fursa na kila atakeye kuja nakuoneshwa kuwa ni awa wamefanya kazi hii hakuna atakayeamini na hii itatoa fursa kwa mabinti wengine walioko vyuoni kuiga mfano huu,”ameongeza Dkt. Batlida Buriani Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga.

Dkt. Buriani aliongeza kuwa katika uongozi wake ataangalia namna ya kuwashirikisha wanawake zaidi katika miradi ili kufikia malengo endelevu ya kuwaezesha wanawake kiutalaam lakini pia kiuchumi.

Mhandisi msamimizi wa jengo hilo, Bi. Immaculata Chaula meviambia vyombo vya habari kuwa alijifunza utaalaam wa masuala ya ujenzi katika Chuo Cha Teknolojia Kilichopo Mbeya (MUST) lakini pamoja na kupata taaluma yake hiyo ni ushiriki wake katika kusimamia moja ya ukumbi wa Manispaa hiyo ndio ulipelekea kumwami na kumpa kazi hiyo.

Bi. Chaula aliongeza kuwa baada ya kumaliza masomo yake alianza kuomba kazi kama fundi wa kawaida mitaani na taaluma yake inachangia sana katika ufanisi wa kazi zake na hivyo kuweza kuaminiwa kwa kazi kubwa anayoifanya kwa sasa.

Jengo la kisasa linalojengwa kwa mfumo wa akaunti ya dharula linajengwa kwa mapato ya ndani na mpaka sasa lipo katika hatua za mwisho kukamilika tayari kwa matumizi ya ofisi ya watumishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama.