November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Vijana 189 wahitimu mafunzo ya stashahada ya Afya mpwapwa

NA STEPHEN Noel,Mpwapwa

VIJANA wapatao 189 wamehitimu mafunzo ya stashahada ya Afya ya wanyama na uzalishaji Katika kampasi ya tasisi ya wakala wa mafunzo ya mifugo Lita ilioko wilayani Mpwapwa.

Akisoma taarifa kituo hicho meneja wa kampasi hiyo,John Kirway amesema kufuatia kuwapo Kwa wanachuo hao Katika kampasi hiyo kumewasaidia Wananchi wanaoizunguka tasisi hiyo Kwa kuwasaidia kutibu wanyama wao na kuwapa elimu ya ufugaji bora.

Kirway amesema zaidi ya mifugo 200 iliweza kuhudumiwa Kwa magonjwa kama ndigana Kali,minyoo na magonjwa mengine yanayowapata wanyama Katika kata za Mpwapwa mjini,Vighawe ,na Berege. “Kwa kweli wakazi wa kata hizi walinufaika wanachuo hawa Kwa ule mpango wa mafunzo nje ya chuo hivyo mifugo ya wakazi hao iliboreka lakini pia Jamii ilipata mafunzo

“Aidha amesema kuwa tasisi hiyo ni miongoni mwa tasisi nane zilizoko chini ya wizara mifugo na uvuvi ambayo ndio kamapasi kongwe hapa Nchini iliyo anzishwa mwaka 1936,”amesema.

Amesema kufuatia ukongwe huo pia miundo Mbinu yake mingi imechaa na inahitaji ukarabati mkubwa.Kwa upande wake mgeni Rasmi Katika maafali hiyo ya 86 Martino Somba amliwataka wahitimu hao kuweza kutumia Elimu waliyoipata kukabiliana na changamoto ya Ajira ,ambayo imekuwa ndio Kikwazo Kwa vijana wengi kushindwa kufikia malengo yao.

Pia amewashauri vijana kuweza kuachana na tabia ya kufanya kazi mmoja mmoja bali wajiunge kwenye Vikundi Ili iwe rahisi kuweza kupata mikopo kirahisi na kuweza kuendelea ndoto zao za kimaisha.

Martino ambae ni kaimu meneja wa NMB tawi la Mpwapwa aliiahidi kuisaidia tasisi hiyo kuweza kuwapatia vifaa vya michezo na vifaa vya TEHAMA.

Mmoja wa wazazi walio hudhuria maafali hiyo CPA Abiniel Kilas aliwataka vijana hao kuweza kulinda maadili na kuwa nidhamu ya pesa kuzitumia Kwa malengo yaliyo kusudiwa.Pa alitoa wito Kwa wazazi kuweza kuwasaidia vijana hao mitaji Ili waweze kufikia ndoto zao Mwisho.