Na Penina Malundo, Timesmajira
Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imetoa ufadhili wa mafunzo ya muda mfupi kwa wanawake 3000 jijiji Dodoma, yatakayotolewa katika Chuo cha VETA Dodoma.
Akizungumza jana, tarehe 24 Machi, 2025 wakati wa hafla ya uzinduzi wa mafunzo hayo yanayotolewa kupitia kikundi cha Wanawake na Samia, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mheshimiwa Rosemary Senyamule amemshukuru Mkurugenzi Mkuu wa VETA, CPA Anthony Kasore kwa ufadhili wa mfunzo hayo.
Senyamule amesema wanawake wengi, hawana ujuzi, hivyo mafunzo ya stadi kwao ni muhimu ili kuwawezesha kujiajiri au kuajiriwa.

“Dodoma sasa ni mji wa kitalii na watu wengi wanakuja kwa ajili ya kupata huduma sa Kiserikali. Wapo wengine kutoka mataifa mbalimbali. Hivyo tunahitajika kutoa huduma za kiwango cha kimataifa na hilo linawezekana ikiwa tutapata mafunzo,” Senyamule amesema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa wanawake na Samia Mkoa wa Dodoma,Fatuma Madidi ametoa pongezi kwa Mkurugenzi Mkuu wa VETA na Mkuu wa chuo cha VETA Dodoma kwa kuridhia mafunzo hayo kutolewa kwa wanwake wa Dodoma kupitia chuo cha VETA Dodoma.
“Ukimsomesha mwanamke umesomesha jamii nzima, tunaahidi kuwa watulivi na kujifunza kwa bidii,” Madidi amesema.

Mkurugenzi Mkuu wa VETA CPA Anthony Kasore amesema VETA itagharamia mafunzo hayo kwa wanawake na Samia na kuongeza kuwa anaamini ujuzi watakaoupata utawasaidia kuendesha shughuli zao za uzalishaji na kujingiizia kipato.
More Stories
Prof.Muhongo apongezwa kuleta majadiliano sekta ya elimu Musoma
Ntiboneka:Mashirika wekezeni katika kubadilisha fikra za vijana,wanawake
Simbachawene:Watendaji wakuu acheni kuwaona wakaguzi wa ndani kama maadui