March 19, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

VETA kuja na zana za kisasa za kufundishia

Na Penina Malundo, Timesmajira 

Mkurugenzi wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Dkt Abdallah Ngodu amesema Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (VETA) kimejipanga kuja na zana za kisasa za ufundishaji katika vyuo vyake.

Ameyasema hayo leo wakati akizungumza kwenye Kongamano la miaka 30 ya VETA inayofanyika Ukumbi wa Ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar,Mkurugenzi wa Elimu ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), Dk. Abdallah Shabani amesema mbali na zana hizo watafanya mabadiliko makubwa ya kuja na walimu wenye uwezo wa kufundisha mafunzo yanayoendana na teknolojia ya kisasa.

Amesena watashirikiana na serikali pamoja na wadau kuhakikisha wanapata vifaa vya kisasa na walimu wenye uwezo wa kufundisha mafunzo yenye tija kwa ulimwengu wa kisasa pamoja na kuangalia suala la wenye uhitaji maalum (walemavu).

Amesema  baadhi ya changamoto zinazokikumba chuo hicho ni kuendelea kutumia mifumo ya kufundishia iliyopitwa na wakati kama vile matumizi ya typewriter wakati ulimwengu tuliopo sasa kila sehemu inatumika kompyuta.

Miongoni mwa walemavu hao ni kijana Joseph Joachim Mtei ambaye amezaliwa bila mikono lakini baada ya kupata mafunzo ya VETA sasa hivi ni msanifu majengo anayetarajia kuhitimu mafunzo yake Desemba mwaka huu.