Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Afisa Madini Mkazi Kahama, Mhandisi Jeremiah Hango amesema kuwa Uzalishaji wa dhahabu umeongezeka kwa kasi kutokana na usimamizi mzuri, sheria na taratibu zilizowekwa na Tume ya Madini.
Mhandisi Hango aliyasema hayo tarehe 14 Februari, 2022 baada ya timu ya Wataalam kutoka Tume ya Madini na Imaan Media kutoka Morogoro kutembelea mgodi wa Bulyanhulu uliopo Halmashauri ya Wilaya ya Msalala na kujionea shughuli za uchenjuaji wa
Alisema kuwa, kuanzishwa kwa masoko ya madini nchini hasa kwenye mkoa huo wa kimadini kumekuwa na mafanikio makubwa kutokana na shughuli za biashara kufanyika sokoni.
“Tumekuwa tukivuka lengo kwenye ukusanyaji wa maduhuli ambapo kwa miezi sita iliyopita kwa mwaka wa fedha 2021/2022 tumekusanya asilimia 110 kupitia shughuli mbalimbali za uzalishaji wa dhahabu,”alisema Mhandisi Hango.
Naye Mkuu wa Uchenjuaji wa dhahabu kutoka Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu Mhandisi Enock Edward alisema kuwa usalama, utunzaji wa mazingira na mabaki yatokanayo na kemikali ni kipaumbele kikubwa kwa usalama wa Wafanyakazi.
More Stories
Mjumbe wa Baraza UWT ahimiza wananchi kuwachagua viongozi wa CCM
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa