Na Israel Mwaisaka,Nkasi
JUMUIA ya Wanawake (UWT) ya CCM wilaya Nkasi mkoani Rukwa kupitia kikundi cha TUPENDANE umezindua mfuko wa pamoja utakaowawezesha wajasiliamali wadogo wenye lengo la kujikwamua kiuchumi kukopa na kupata mitaji ya kuendesha shughuli zao za kiuchumi.
Uzinduzi wa mfuko huo ni kwenda sambamba na kauli ya Mwenyekiti wa CCM taifa na Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt,Samia Suluhu Hassan ya “siasa ni uchumi na uchumi ni siasa” katika mpango mathubuti wa Wanawake kujikomboa kiuchumi na kisiasa
Akizindua mfuko huo mwenyekiti wa CCM wilaya ya Nkasi Keissy Aljabri Sudi aliwapongeza Wanawake hao kuubuni mfuko huo na kuwa lengo la CCM na serikali yake ni kutaka makundi mbalimbali ya kijamii yanajikwamua kiuchumi ikiwemo kundi kubwa la Wanawake.
Amesema kuwa maendeleo ni mchakato na wengi ukosa mitaji kujiendeleza na kuwataka sasa kuutumia mfuko huo kukopa na kujiendeleza kiuchumi ikiwa ni pamoja na kujakikisha kuwa unakua endelevu hasa kwa kurejesha mikopo kwa wakati.
Uzinduzi wa mfuko huo ulikwenda sambamba na harambee ya kuukuza mfuko huo ambapo wadau walichangia Milioni 8,254,099,000 ambapo fedha taslimu Ni Mil.6.54 na ahadi ni Mil.2.2.
Mmoja wa Wadau wa chama hicho Salumu Kazukamwe alichangia Mil.6 huku wengine wakichangia kiasi kingine kilichopatikanika na kuuwezesha mfuko huo kuweza kupata fedha fedha nyingi na Wanawake kuwa na uwezo mkubwa wa kukopa na kuendesha shughuli mbalimbali za kiuchumi.
Mwenyekiti wa UWT wilaya Nkasi Beatrice Nguwa kwa upande wake amewataka Wanawake kushikamana ipasavyo katika kipindi hiki na kuutumia muda mwingi katika kupeana ujuzi wa mambo mbalimbali katika kufikia hazima yao ya kujikwamua kiuchumi badala ya muda huo kuutumia kwa mambo yasiyo na msingi,huku akiwashukuru wachangiaji wote walioukuza mfuko wao kupitia harambee waliyoifanya
Uzinduzi wa mfuko huo uliofanyika katika ukumbi wa chuo cha Mtakatifu BAKHITA mjini Namanyere uliwajumuisha viongozi mbalimbali wa chama ngazi ya wilaya kwa kuwashirikisha Wadau wengine wa maendeleo.
Mwisho
More Stories
TTCL yafanya maboresho katika huduma zake
HGWT yawataka wazazi na walezi kulinda watoto dhidi vitendo vya ukatili
ACT-Wazalendo,waitaka Polisi kutobeba chama kimoja